Mwenyekiti wa Bunge la Katiba
Dodoma. Kura za awali katika Kamati 10 kati ya
12 za Bunge Maalumu la Katiba, zinakipa wakati mgumu Chama Cha
Mapinduzi,(CCM) kutekeleza azma yake inayotajwa kuwa ni kufumua Rasimu
ya Katiba, ili kuondoa mapendekezo ya Muundo wa serikali tatu, baada ya
wajumbe wa Zanzibar kukwamisha upatikanaji theluthi mbili.
Kwa mujibu wa taarifa za kamati, ambazo tangu juzi
zimeanza kutolewa katika sura ya kwanza na sita zinazungumzia Muundo wa
Muungano, wajumbe kutoka Zanzibar kwa sasa ndiyo kikwazo kikubwa kwa
CCM.
Hata hivyo, uamuzi ya mwisho kuhusu Muundo wa
Serikali, kati ya mbili au tatu, unatarajiwa kujulikana Alhamisi wiki
ijayo, wakati kamati zote zitakapowasilisha taarifa zao na kupigwa tena
kura kwa wajumbe Tanzania Bara peke yao na Zanzibar peke yao.
Iwapo wajumbe wa Zanzibar wakiitetea kwa theluthi
mbili kama sasa, mapendekezo ya muundo wa serikali tatu ndiyo
yatakayopelekwa kwa wananchi.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na gazeti hili,
baadhi ya wenyeviti wa kamati hizo, Stephen Wassira, Ummy Mwalimu, Anna
Abdalah na Paul Kimili, walitaja moja ya vifungu ambavyo vimeshindwa
kupata theluthi mbili kuwa ni ibara ya kwanza kifungu cha kwanza.
Akizungumza jana Wassira ambaye ni Mwenyekiti wa
Kamati Namba Sita alisema kwamba katika kamati yake ibara hiyo
imeshindwa kupata theluthi mbili, ili kuweza kufanyiwa marekebisho.
“Lakini huu siyo mwisho kama nilivyosema awali,
tukirudi bungeni tutapiga kura kwa wajumbe wote na ndiyo itakuwa na
uamuzi wa mwisho kama muundo wa Muungano utakuwa na Serikali tatu ama
mbili, ambao utapelekwa kwa wananchi,” alisema Wassira.
Jussa, Lissu- tumeibana CCM
Jussa alisema: “Kwa taarifa za matokeo tulizonazo
katika Kamati Namba 1, 2, 3, 4, 6, 10, 11 na 12 mapendekezo ya
kubadilisha Rasimu katika ibara hizo mbili yamekwama. Kama CCM
wakichakachua sura ya kwanza na sita, maana yake ni kwamba hapa hakuna
Katiba, hakuna kura ya maoni na hakuna mwafaka.”
Vifungu hivi pia kwa mujibu wa wenyeviti wa kamati
nyingine, isipokuwa kamati ya Tano, ambayo inaongozwa na Hamad Rashid,
havikupata kura theluthi mbili na hivyo kubaki kama vilivyo kwenye
rasimu.
Naye Lissu alisema kwa sasa CCM ndiyo inaweza
kuanza mkakati wa kuvuruga Bunge kwani tayari wamejua hawana theluthi
mbili ya Zanzibar ili kubadili Rasimu kama wanavyotaka.
No comments:
Post a Comment