PICHA ZA UFUNGUZI WA MAONYESHO YA NANENANE NA UFUNGUZI WA MAADHIMISHO YA WIKI YA UNYONYESHAJI KITAIFA INAYOFANYIKA MKOANI DODOMA


Wanafunzi wa shule ya msingi ya  Nhinhi wiyani Chamwino wakicheza ngoma ya kabila la kigogo wakati wa Uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya Unyonyeshaji maziwa ya mama kwa mtoto kwa miezi sita yaliyofanyika katika kijiji cha Nghwenda katika mfurulizo wa wiki ya hiyo inayofanyika kitaifa mkoani Dodoma

Mtoto Mwenye umri wa miaka saba akingoza kikundi cha nyota katika upigaji na uchezaji wa ngoma wakati kikundi hicho kilipokuwa kikiwatumbuiza wakili, wafugaji na watu mbalimbali wanaohudhuria maonyesho ya Nanenane yanayoendelea kikanda mkoani Dodoma kabla ya Mkuu wa mkoa huo kuyafungua Rasmi maonyesho hayo.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Chiku Gallawa, akiangalia mazao aina ya Uwele ambayo inashauriwa kulimwa kwa wingi katika mikoa ya kanda ya kati kutokana na mazao hayo kustahimili ukame.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Chiku Gallawa akipokea Nyanya aina ya NOR FI toka kwa Mkuu wa kitengo cha mafunzo ya kilimo cha kisasa wa Clabu ya Vijana wasomi wa Elimu ya juu Agrikolas Masigati wakati mkuu huyo wa moa alipotembelea Banda la maonyesho la Wilaya ya Kondoa katika viwanja vya maonyesho ya nanenane jana

Nahodha wa Timu ya mpira wa miguu ya Watoto wa Town ya kijiji cha Nhinhi Babuu Abel akipokea zawadi ya Mpira toka kwa Katibu Tawala wa mkoa wa Dodoma Rehema Madenge baada ya timu yake kushika nafasi ya pili kwenye mchezo wa fainali wa maadhimisho ya siku ya unyonyeshaji ambapo nafasi ya kwanza ilienda kwa Small Boys iliyopata zawadi ya Jezi.

Baadhi ya wanawake na wanaume wakiwa na watoto wao kwenye uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya Unyonyeshaji kitaifa inayoendelea mkoani Dodoma yaliyofanyika katika kijiji cha Nghwenda kata ya Nhinhi wilayani Chamwino.

PICHA NA JOHN BANDA 


No comments:

Post a Comment