TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Timu
ya Taifa ya Tanzania chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) sasa itaivaa
Misri kwenye raundi ya pili ya michuano ya kuwania tiketi ya kucheza
Fainali za 10 za Afrika kwa vijana chini ya miaka 17 zitakazofanyika
mwakani nchini Morocco.
Awali
Serengeti Boys ilikuwa icheze raundi ya kwanza dhidi ya Kenya, mechi
ya kwanza ikichezwa Septemba 9 mwaka huu jijini Dar es Salaam. Hata
hivyo, Shirikisho la Mpira wa Miguu la Kenya (FKF) jana lilituma
taarifa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) likielezea kujitoa
kwenye michuano hiyo.
Serengeti
Boys itaanzia nyumbani Oktoba 14 mwaka huu, wakati ya marudiano
itachezwa nchini Misri kati ya Oktoba 26-28 mwaka huu. Mshindi baada ya
mechi hizo mbili ataingia raundi ya tatu ambayo ndiyo ya mwisho kabla
ya kwenda Morocco.
Katika
raundi ya tatu ambayo mechi zake zitachezwa katikati ya Novemba na ya
marudiano mwisho mwa mwezi huo, mshindi kati ya Tanzania/Misri atacheza
na mshindi wa mechi ya Congo Brazzaville dhidi ya Msumbiji/Zimbabwe
ambazo zinapambana katika raundi ya kwanza.
Wachezaji
wanaounda kikosi cha Serengeti Boys chini ya Kocha Jakob Michelsen ni
makipa Abdallah Bakar (Mjini Magharibi), Hamad Juma (Azam) na Peter
Manyika (JKT Ruvu).
Mabeki
ni Abdallah Salum (Mjini Magharibi), Basil Seif (Morogoro), Hassan
Mganga (Morogoro), Ismail Gambo (Azam), Mgaya Abdul (Azam), Miraji
Selemani (Polisi Morogoro), Miza Abdallah (Kinondoni), Mohamed Hussein
(Azam), Pascal Matagi (Dodoma) na Paul James (Kinondoni).
Viungo
ni Farid Musa (Kilimanjaro), Hussein Twaha (Coastal Union), James
Mganda (Kipingu Academy), Mbwana Ilyasa (Simba), Mohamed Haroub
(Zanzibar), Mohamed Kapeta (Kinondoni), Mudathiri Yahya (Azam), Mzamiru
Said (Morogoro) na Selemani Bofu (JKT Ruvu).
Washambuliaji
ni Abdallah Kisimba (Mwanza), Calvin Manyika (Rukwa), Dickson Ambunda
(Mwanza), Joseph Lubasha (Azam), Kelvin Friday (Azam) na Salvatory
Nkulula (Kipindu Academy).
MCHEZAJI AOMBEWA ITC UJERUMANI
Chama
cha Mpira wa Miguu cha Ujerumani (DFB) kimetuma maombi ya kupatiwa
Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa ajili ya mchezaji Robert
Makanja ili aweze kucheza mpira wa miguu nchini humo.
DFB
imetuma maombi hayo Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ili
kumwezesha mchezaji huyo kuichezea timu ya TUS Ahausen, Hessischer
FuBall-Verband ambayo hata hivyo haikuelezwa iko ligi ya daraja gani
nchini humo.
Kwa
mujibu wa Mkuu wa Mashindano wa DFB, Markus Stenger, Mtanzania huyo
ameombewa hati hiyo kama mchezaji wa ridhaa kwa maelezo kuwa hakuwahi
kusajiliwa na klabu yoyote nchini.
TFF
inafanyia kazi maombi hayo na hati hiyo itatolewa mara baada ya
taratibu husika kukamilika ikiwemo kubaini kama kweli mchezaji huyo
hakuwahi kusajili na klabu yoyote hapa nchini.
Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
No comments:
Post a Comment