Jumla ya watu 251 wameuwawa katika ajali zilizohusisha usafiri wa
Bodaboda jijini Dar es salaam katika kipindi cha miezi mitatu
iliyopita jijini.
Katika ajali hizo zaidi ya watu 1289 wamepata majeraha huku wengine wakipata ulemavu wa kudumu.
Wadau wa Usalama barabarani wameainisha kuwa, biashara holela kwa
madereva wasio na mafunzo NI chanzo cha ongezeko la ajali vyombo hivyo
vilivyoshika kasi kipindi cha hivi karibuni.
Baadhi ya waendesha vyombo hivyo vya usafiri wamekana kuwa wao
pekee ndo chanzo cha ajali bali ni kukosekana kwa umakini baina ya
mamlaka za usalama pamoja na wamiliki wa vyombo vya usafiri
Kamanda poilisi kikosi cha usalama barabarani kamanda Mohammed
Mpinga, ikiwa ni moja ya mbinu za kukabiliana na ajali kwa
kushirikiana na wadau wa vyombo vya usafiri wamekuatana jijini Dar es
salaam na kuzindua mafunzo kwa madereva zaidi ya elfu moja
yatakayotolewa bure kwa yeyote aliye na nia ya kuwa dereva bora wa
bajaji na bodaboda jijini hapa.
Kwa upande mwingine wizara ya mambo ya ndani bado ina kazi kubwa
ya kufanya kwenye upenyo wa biashara huria na bado kuna mwanya wa
uzembe katika kusimamia kiuhakika usalama wa vyombo vya usafiri, Nizar
Jivani ni Rais wa chama cha wamiliki wa bodaboda na bajaji AAT.
Ajali za barabarani licha ya maangalizo mbalimbali yanayoatolewa
zimeendelea kuwa wimbo wa kila uchao huku maisha ya wananchi
yakiendelea kuteketea, na kubwa ikiwa ni ongezeko la kizazi tegemezi
kutokana na wengi kuachwa wakiwa na ulemavu .
No comments:
Post a Comment