Watu 13 wamefariki dunia na wengine 18 kujeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea wilayani Musoma, mkoani Mara.
Ajali hiyo ilitokea juzi jioni katika kijiji cha Mkiringo nje kidogo ya Manispaa ya Musoma.
Katika
ajali hiyo, watu tisa walikufa papo hapo fariki huku wanne wakati
wakipatiwa matibabu katika Hospitali ya Mkoa wa Mara mjini Musoma.
Miongoni
mwa watu walifaki dunia ni pamoja na askari wawili wa Jeshi la Kujenga
Taifa (JKT) kikosi cha Rwamkoma huku wengine 15 wakiendelea na matibabu
katika hospitali hiyo.
Mashuhuda
wa ajali hiyo na baadhi ya abiria walikuwa katika gari hilo dogo aina
ya Toyota Hiace lenye namba za usajili T 123 CAE lililokuwa likitokea
mjini Musoma kwenda kijiji cha Nyamuswa wilayani Bunda, walisema kuwa
chanzo cha ajali hiyo ni kujaza abiria kupita kiasi na mwendo kasi.
Walisema kuwa mwendo kasi ulisababisha kupasuka gurudumu la nyuma upande wa kulia kisha kupinduka na kuua watu tisa papo.
Julius
Masato, shuhuda wa ajali hiyo, alisema aliliona gari hilo likiwa katika
mwendo wa kasi likiwa na abiria wengi kabla ya gurudumu kupasuka na
kupinduka.
Kaimu
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Mara, Dk. Joseph Nyamagwira,
alisema kutokana na baadhi ya majeruhi hao kujeruhiwa vibaya na wengine
kuvunjika viungo vyao vya mwili, watalazimika kuhamishiwa haraka katika
Hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza kwa ajili ya kupatiwa
matibabu ya uhakika.
Dk.
Nyamagwira alisema kuwa baadhi marehemu ambao wamehifadhiwa katika
chumba cha maiti katika hospitali hiyo ni pamoja na Esther John na
Emmanuel Joseph, ambaye alikuwa dereva wa Hiace hiyo.
Kwa
mujibu wa Dk. Nyamagwira, miili mingine inayohifadhiwa katika hospitali
ya mkoa ni ya Pendo James na mtoto wake, Joseph Richard pamoja na
Razack Shaban, wakazi wa kijiji cha Nyamuswa.
Wengine
ni Hamis Kanyoro Richard, Makuri Magori, wakazi wa Bisarya; Nyamazare
John, Innocent Kweka, Richard Said Dogori, Hassan Masoke na mmoja ambaye
ametambulika kwa jina moja la Isaac. Wote hawajafahamika meneo
wanayotoka.
Baadhi
ya ya majeruhi katika ajali hiyo wametajwa kuwa ni Betty Ngutu,
Elfansia Kamanzi, wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Chief Ihunyo.
Wengine ni Busegwe, Mather Makori na wengine ambao hali zao ni mbaya hawajafahamika.
Pia
wamo Hamis Isaac na Beatrice Sirima Isaac na Sirima walisema kuwa baada
ya kufika katika eneo la Mkiringo gari lao lililokuwa katika mwendo
kasi lilijaribu kulikwepa gari lingine na ndipo lilipopasuka gurudumu la
nyuma na kuchomoka wakiwa katika mteremko na gari kupinduka mara tatu.
Kuhudi
za kumpata Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara, Absalom Mwakyoma,
hazikufanikiwa kutokana na simu zake zote za kiganjani kufungwa.
No comments:
Post a Comment