TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Septemba 6, 2012
Kombaini
ya Tanzania ya Copa Coca-Cola imeshika nafasi ya pili katika kambi ya
kimataifa ya michuano hiyo inayoendelea jijini Pretoria, Afrika Kusini.
Tanzania imemaliza mechi za kambi hiyo kwa kufikisha pointi 14.
Ilicheza
mechi yake ya mwisho jana (Septemba 5 mwaka huu) dhidi ya Malawi na
kutoka suluhu, matokeo yaliyoifanya ifikishe pointi 14. Zambia ndiyo
iliyokamata nafasi ya kwanza kwa kufikisha pointi 15.
Mechi
hizo zilichezwa kwa mtindo wa ligi baada ya nchi nyingine kushindwa
kwenda Afrika Kusini kutokana na kuchelewa kupata viza za kuingia za
kuwawezesha kuingia nchini humo.
Mbali
ya Tanzania, nchi nyingine zilizowahi kambi hiyo ni Kenya, Uganda,
Nigeria, Malawi, Msumbiji, Zimbabwe, Zambia na timu mchanganyiko katika
kambi hiyo (CEWA).
Katika
mechi zake Tanzania ilitoka suluhu na Nigeria, ikafungwa 3-2 na Kenya,
ikaichapa Zimbabwe 3-0, ikailaza CEWA 3-0, ikaifunga Msumbiji 2-0,
ikashinda 2-0 dhidi ya Uganda na ikafungwa 1-0 na Zambia.
Wachezaji
wawili wa Tanzania wamechaguliwa kwenye kombaini ya kambi hiyo (Dream
Team). Wachezaji hao ni mfungaji bora Basil Seif ambaye ana mabao sita
na kipa bora Tumaini Baraka. Pia Sylvester Marsh wa Tanzania
amechaguliwa kuwa kocha bora katika kambi hiyo.
Makocha
watano kutoka timu ya Chelsea ya Uingereza wanaanza kutoka mafunzo leo
(Septemba 6 mwaka huu) ambapo yatamalizika kesho (Septemba 7 mwaka
huu) na timu zitarejea nyumbani Septemba 8 mwaka huu. k.
Robert
Luke Udberg, Russel William Banyard, Oliver Staurt Woodall, Shane
Jason Hughes na Dean Aaron Steninger kutoka Chelsea FC Foundation ndiyo
wanaounda jopo hilo la makocha.
MKATABA WA UDHAMINI KUSAINIWA SEPT 11
Mkataba
wa udhamini wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara ambayo itadhaminiwa tena
Vodacom utasainiwa Jumanne (Septemba 11 mwaka huu) kwenye ofisi za
kampuni hiyo jijini Dar es Salaam.
Taarifa rasmi juu ya muda wa kusaini na pande zitakazoshuhudia hafla hiyo itatolewa hivi karibuni.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
No comments:
Post a Comment