Hezbollah yaitisha maandamano zaidi

Kiongozi wa kundi la Hezbollah nchini Lebanon, amesema kuwa marekani ni sharti ikubali lawama kuhusiana na filamu iliyotayarishwa nchini humo ambayo inaidhalilisha dini ya kiislamu na kusababisha ghadabu katika mataifa mengi ya kiislamu.

Kiongozi wa Hezbollah, Sheikh Hassan Nasrallah, alitoa wito kufanyika kwa maandamano ya wiki nzima, sio tu katika balozi za Marekani bali pia kuzishinikiza serikali za kiislamu kuelezea ghadhabu dhidi ya Marekani.

Huku maandamano ya kuipinga Marekani yakiendelea kuhusiana na filamu hiyo katika mataifa kadhaa, mtu mmoja aliuwawa katika makabiliano na maafisa wa usalama nje ya ubalozi mdogo wa Marekani katika mji wa Karachi, Pakistan.

Maandamano katika balozi nyingi za Marekani yamekuwa yakiendelea kuhusu filamu hiyo iliyotengezwa nchini Marekani na kumdhihaki Mtume Muhammad.

Katika hotuba yake iliyopeperushwa kupitia kituo cha televisheni cha kundi hilo, Al-Manar, Sheikh Nasrallah alitoa wito wa kufanyika maandamano zaidi.

Maandamano ya kwanza yatafanyika hii leo Kusini mwa Beirut eneo ambalo ni ngome kubwa ya Hezbollah.

Sheikh Nasrallah aliitaja filamu hiyo kama hatari sana na kusema ni matusi makubwa kuwahi kutolewa dhidi ya uisilamu. Alisema ni matusi makubwa hata kuliko kitabu kilichoandikwa na Salman Rushdie (Satanic Verses) kikimkejeli Mtume Muhammad na ambacho kilichapishwa na gazeti moja nchini Denmark mwaka 2005.

No comments:

Post a Comment