Makaburi ya siri yagunduliwa Tana

Hali ya taharuki inaendelea kutanda katika eneo la Tana Delta Pwani ya Kenya ambako Polisi wanasema wamegundua makaburi mawili ya siri.

Idadi ya maiti waliozikwa kwenye makaburi hayo yaliyogunduliwa katika kijiji cha Ozhi ambacho kimekuwa kitovu cha ghasia hizo,haijulikani kulingana na polisi wala haijutambulishwa.

Kwa sasa polisi wameomba idhini ya mahakama kuweza kufukua makaburi hayo.

Hapo jana nyumba ishirini ziliteketezwa moto na watu wasio julikana.

Zaidi ya watu 100 wameuawa katika mapigano kati ya wakulima na wafugaji wanaozozania ardhi na maji katika eneo hilo.

Afisa mkuu wa polisi mkoani pwani, Aggrey Adoli, ameiambia BBC kwamba bado wanasubiri kibali cha mahakama kuwaruhusu kufukua na kubaini miili hiyo.

Kuna madai kuwa wanasiasa ndio waliochochea ghasia hizo huku heka heka za uchaguzi mkuu nchini zikiwa zimenza. Uchaguzi huo utafanyika mwezi Machi mwaka ujao.

Ramani ya Kenya

Waekezaji wa nje na ndani ya nchi wamekuwa wakitafuta vibali vya kumiliki ardhi katika eneo hilo kwa lengo la kufanya kilimo na kutengeza kawi inayotokana na mimea.

Na kwa hivyo kuchaguliwa kushikilia wadhifa wowote serikalini kunampa mwanasiasa ushawishi mkubwa sana katika eneo hilo.

Kuna wasiwai kuwa huku uchaguzi ukikaribia, ushindani wa kisiasa heunda ukachochea ghasia kuzuka tena kama ilivyokua katika uchaguzi wa mwaka 2007

No comments:

Post a Comment