MAREFA WATANO TU WA TANZANIA NDIO WANATAMBULIWA FIFA

Israel Mujuni Nkongo, mmoja
wa marefa wa FIFA

KWA sasa Tanzania ina marefa watano tu wanaotambuliwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), kati yao mmoja mwanamke mmoja tu, Judith Gamba kutoka Arusha.

Marefa wa kiume ni Isarel Mujuni Nkongo (Dar es Salaam), Charles Orden Mbaga (Dar es Salaam), Waziri Shekha (Z’bar) na Ramadhani Kibo (Z’bar).

Aidha, marefa wasaidizi, maarufu kama washika vibendera wanaotambuliwa na FIFA ni 10, kati yao wawili wanawake, ambao ni Sada Tibabimale (Mwanza) na Mwanahija Makame (Z’bar), wakati wanaume ni Hamisi Chang’walu (Dar es Salaam), John Kanyenye (Mbeya)

Jesse Rasmo (Morogoro), Samuel Mpenzu (Arusha), Ferdinand Chacha (Kagera), Hamisi Maswa (Z’bar), Josephat Bulari (Z’bar) na Ramadhan Chinduli (Z’bar).

Marefa hawa ambao huchezesha mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika, hatua za awali za Kombe la Mataifa ya Afrika na Kombe la Dunia, ndio kati yao wanapewa nafasi ya kuchezesha mechi za watani wa jadi, Simba na Yanga.

Lakini mechi ya mwisho ya Ligi Kuu msimu uliopita baina ya wapinzani hao wa jadi, ambayo Yanga ilifungwa 5-0, haikuchezeshwa na marefa wa FIFA, ambao ni Hashim Abadallah aliyesaidiwa na Iddi Maganga na Omar Kambangwa, wote wa Dar es Salaam.

Kabla ya hapo, kwa muda mrefu, mechi hizo za watani zimekuwa zikichezeshwa na Orden Mbaga na Israel Nkongo- baada ya utawala wa Victor Mwandike, Paschal Chiganga na Emmanuel Chaula, ambao waliwapokea Omar Abdulkadir, Nassor Hamdoun na Kanali Issaro Chacha.

No comments:

Post a Comment