Takriban watu 38 wameuawa katika mapigano mapya yaliyozuka eneo la Tana River siku tatu tu baada ya watu 12 wa kabila la Pokomo kuuawa katika mashambulizi yaliyofanya na jamii hasimu ya Orma.
Msemaji wa polisi Eric Kirathe amethibitisha
kuwa polisi 8 ni miongoni mwa waliouawa katika makabilianao hayo
yaliyotokea asubuhi ya leo kusini mashariki mwa Kenya.
Muuguzi akimhudumia mwathiriwa wa ghasia Tana River
Kulingana na shirika la misaada la Red Cross, nyumba zimeteketezwa moto baada ya kijiji hicho kuvamiwa na zaidi ya watu mia tatu.
Tukio hili linajiri siku kadhaa baada ya mashambulizi mengine kutokea kwenye eneo hilo la Tana Delta na kusababisha vifo vya karibu watu kumi na saba.
Jamii za wafugaji wa kuhama hama na wakulima zimekuwa zikizozania rasilmali kwenye eneo hilo la Tana Delta lililo na rutuba nyingi na maji.
Polisi kwa usihirikiano na shirika la msalaba mwekundu wameweza kuokoa manusura. Inaarifiwa watu wameanza kuhama eneo hilo la Tana River kukimbilia usalama wao.
Ramani ya Kenya
''Hali inaendelea kuwa mbaya. Hatua zinapaswa kuchukuliwa kwa dharura.'' alisema afisaa mkuu mtendaji wa shirika la Msalaba mwekundu. Abbas Gullet
Bwana Gullet alikadiria idadi ya waliofariki kuwa watu 39 na kusema kuwa watoto 8 ni miongoni mwa waliouawa.
Msemaji wa polisi naye alikadiria idadi ya
waliofariki kuwa watu 30.Mwezi jana zaidi ya watu 50 waliuawa katika
mapigano mengine kati ya jamii za Pokomo na Orma.
Hizi ni ghasia mbaya zaidi kushuhudiwa hivi karibuni tangu zile za mwaka 2007 kufuatia uchaguzi uliozua utata mkubwa.
No comments:
Post a Comment