NBS Yaongeza Siku Ya Wananchi Ambao Hawajafikiwa Na Makarani Ili Wahesabiwe
Ofisi
ya Taifa ya Takwimu (NBS) imeongeza mbele tarehe za kumaliza kazi ya
sensa ya watu na makazi hadi Jumamosi ya tarehe 8 septemba mwaka huu ili
kuhakikisha kuwa kila mwananchi aliyebaki anahesabiwa.
Kauli
hiyo imetolewa leo(jana) na Kamishna wa Sensa kutoka NBS Hajjat Amina
Mrisho Said wakati akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es salaam
kuhusu masuala mbalimbali yaliyohusu kazi nzima ya kuhesabu watu na
makazi inaendelea katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
Alisema
kuwa ni vema wananchi ambao hawajafikiwa na makarani wa sensa watoe
taarifa katika Ofisi za Serikali za Mitaa au Ofisi ya Taifa ya Takwimu
kwa ajili ya kuhesabiwa.
Hajjat
Amina alisema taarifa zinazotakiwa ni pamoja na taarifa za wanakaya
waliolala katika kaya yao usiku wa kuamkia tarehe 26 Agosti mwaka huu.
Alitoa
wito kwa wale ambao hawajaandikishwa hadi hivi sasa wanatakiwa watume
taarifa kwa namba 2122724, 0754583415, 2129622 ,0713335429,0713574622 na
0713312699 .
Hajjat
aliongeza kuwa katika taarifa watakazopeleka ni vema wakaeleza mitaa au
kijiji au kitongoji gani walipo ili iwe rahisi kwa NBS kutambua karani
mhusika na kumwelekeza afanye kazi hiyo.
Aidha
, Kamishna hiyo alisema kuwa malipo ya makarani yalishafanyika kwa
awamu ya kwanza kulingana na mkataba na wanataraji kuwalipa awamu ya
pili mara baada ya kazi zao kuhakikiwa na wasimamizi wao.
Aliongeza kuwa kwa wasimamizi watalipwa baada ya kazi zao kukamilika na kuhakikiwa na waratibu katika ngazi za wilaya.
Kuhusu
malipo ya wenyeviti wa vijiji , vitongoji na mitaa ,alisema fedha zao
wasishapelekwa siku nyingi na maelekezo ya namna ya kuzigawa yalipelekwa
kwa waratibu wa Sensa wa mikoa na wilaya ambao walipaswa kuwa
wameshalipa ili kuepuka manung’uniko.
Katika
hatua nyingine Kamishna wa Sensa huyo amewaonya kuwa Karani yoyote
atakayechakachua taarifa na ikathibitika hilo atachukuliwa hatua kwa
mujibu wa Sheria na kuongeza kuwa NBS inafuatilia taarifa kutoka Dodoma
eneo la Kisasa kuwa kuna Karani amekwenda kwenye kaya lakini alikuwa
haulizi maswali.
Wakati
huo huo Kamishna wa Sensa Hajjat Amina alisema kuwa wale viongozi wengi
waliokuwa wakiwa hamasisha wenzao wasihesabiwe , wamehesababiwa kwa
hiari baada ya kutoa ushirikiano wa kutosha ikiwemo kuacha taarifa
muhimu zilizohitajiwa ikiwemo zile zilihitajika katika madodoso. Kwa
wale ambao hawakuwakuta waliweka alama maalum ili wawarudie mara ya
pili.
No comments:
Post a Comment