Njama ya mashambulizi yatibuliwa Kenya
Polisi nchini Kenya wamenasa magwanda
yenye mabomu ya kujilipua pamoja na zana zengine ambazo zilikuwa
zitumike kwa mashambulizi ya kigaidi mjini Nairobi.
Washukiwa wawili wamekamatwa katika msako huo uliofanywa asubihi ya leo katika mtaa wa Eastleigh mjini Nairobi.
Msemaji wa polisi nchini Kenya Eric
Kiraithe anasema kuwa maguruneti kumi na mbili pamoja na bunduki aina ya
AK 47 pia zilinaswa wakati wa msako uliofanywa na polisi mtaani humo.
"tunaamini kuwa silaha hizi zilinuiwa kutumika kufanya mashambulizi ya kigaidi mjini Nairobi'' alisema bwana Kiraithe.
Silaha hizo zinasemekana kufanana na zile
zilizotumika katika mashambulizi ya kigaidi yaliyofanyika nchini Uganda
dhidi ya watu waliokuwa wanatazama fainali ya kombe la dunia mwaka 2010,
ambapo watu 76 waliuawa
Kundi la Al-Shabab lilikiri kufanya mashambulizi
nchini Uganda, wakisema kuwa wanapinga kuhusika kwake na mapambano
dhidi ya kundi hilo nchini Somalia.
Kenya imeshambuliwa karibuni na kundi la al-Shabab baada ya kupeleka vikosi vyake Somalia.
No comments:
Post a Comment