Rais mpya wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud
Rais mpya wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud , amenusurika jaribio la kumuua mjini Mogadishu.
Milipuko miwili imetokea nje la lango la makao
ya rais huyo katika hoteli ya Al-Jazeera wakati rais huyo alipokuwa
anajiandaa kufanya mkutano na waandishi wa habari.
Taarifa zinasema kuwa waziri wa mambo ya nje wa
Kenya Sam Ongeri pia alikuwa katika hoteli hiyo wakati wa shambulizi.
Hata hivyo wawili hao wamenusurika. Inaarifiwa watu wanne wameuawa na
wengine watatu kujeruhiwa.
No comments:
Post a Comment