Mazungumzo kati ya nchi hizo mbili yalifanyika nchini Ethiopia
Sudan na Sudan Kusini zimetia saini makubaliano kuhusu biashara, mafuta na usalama ingawa hazijakubaliana kuhusu mipaka.
Baada ya mazungumzo ya siku ya nne, nchi hizo
mbili zimeafikiana kuruhusu usafirishaji wa mafuta kutoka kusini kupitia
mabomba ya Kaskazini na kuondoa wanajeshi mpakani.
Viongozi wa nchi hizo mbili hatimaye wamekubaliana baada ya mazungumzo ya siku nne mjini Addis Ababa Ethiopia.
Lakin maswala kadhaa muhimu yangali kutatuliwa
ikiwemo kuafikia makubaliano kuhusu mipaka inayozozaniwa ikiwa ni
mojawpao ya kilichosababisha mgogoro ambao nusura utumbukize nchi hizo
kwenye vita mapema mwaka huu.
Baada ya mapigano kuzuka kuhusu mzozo wa mafuta
na mipaka, Umoja wa mataifa ulitishia kuziwekea pande zote mbili vikwazo
ikiwa hazitaafikia makubaliano ya kina.
Wapatanishi wa Muungano wa Afrika wangali
kuthibitisha kuwa makubaliano yameafikiwa lakini rais wa Sudan Omar
al-Bashir na mwenzake wa Kusini Salva Kiir, wanatarajiwa kutia saini
makubaliano hayo hii leo.
Maelezo yametolewa tu kwa mukhtasari lakini
wapatanishi wa pande zote mbili, walisema kuwa wamekubaliana kuhusu eneo
la nchi hizo mbili ambalo halina ulinzi wa kijeshi.
Pia makubaliano ya kiuchumi yaliafikiwa kuruhusu Sudan Kusini kuanza tena shughuli zake za kuzalisha mafuta.
Lakini mwafaka haukupatikana kuhusu eneo linalozozaniwa la Abyei wala mipaka mingine mingi ambayo nchi hizo zinazozania.
Kwa hivyo makubalino hayo hayajaweza kutimiza
masharti ya Umoja wa Mataifa kwa nchi hizo kuafikia mkataba unaotatua
mzozo huo kwa kina.
No comments:
Post a Comment