Marais wa Sudan
na Sudan Kusini hii leo wanaendeleza mazungumzo kuhusu mizozo
iliyowasababisha kukaribia kutumbukia katika vita mapema mwaka huu.
Masuala muhimu katika mkutano huo unaofanyika
nchini Ethiopia ni usalama katika maeneo ya mpakani, ugavi wa mapato ya
mafuta na eneo lenye utata la Abyei.
Baada ya masaa mawili ya mazungumzo siku ya
Jumapili,msemaji wa serikali ya Sudan, Badr El-Din Abdallah, alisema
kuwa hatua zimepigwa kati ya pande zote mbili lakini swala la amani
ndilo bado linazua utata
Umoja wa mataifa umetishia kuziwekea pande zote mbili vikwazo ikiwa hazitaafikia makubaliano na amani ya kudumu
Sudan Kusini ilijipatia uhuru mwaka jana kutoka
kwa Sudan baada ya makubaliano ya amani kumaliza vita vya wenyewe kwa
wenyewe vya zaidi ya miaka kumi.
No comments:
Post a Comment