Taswira Za Uzinduzi Wa Shina La CCM UK Leicester
Bi Mariam Mungula Katibu Mpya wa CCM Tawi la Uingereza akikabidhi kadi kwa wanachama wapya.
CHAMA CHA MAPINDUZI.
TAWI LA UNITED KINGDOM.
Website: www.ccmuk.org E-mail: ccmlondon@gmail.com
CCM UINGEREZA YAFUNGUA SHINA JIPYA LA LEICESTER KWA HOJA NA
KISHINDO
Chama Cha Mapinduzi ,Tawi la Uingereza Jana Tarehe 09.09.12 kimefungua
shina Jipya katika Mji wa Leicester kwa changamoto ya hali ya juu, hoja
nzito na kishindo kikubwa.
Katika ufunguzi huo uliosimamiwa na Katibu Mpya wa Tawi Bi. Mariam
Mungula alisisitiza suala la umoja kwa wana CCM na wanadiaspora kwa
ujumla katika kutoa mchango wao kwa sauti moja ili kuweza kuwa na Nguvu
ya pamoja na kuchangia katika kuboresha ufanisi wa Serikali ya Tanzania
kwenye Nyanja mbali mbali za huduma za kijamii na maendeleo ya kiuchumi
kwa faida ya watanzania wote.
Awali Bi. Mungula alitoa salamu kutoka kwa Mh. January Makamba kama
Katibu wa NEC Siasa na Ushirikiano wa Kimataifa ambae aliwahakikishia
wana CCM Diaspora kuwa , CCM huko nyumbani ,akiwemo Mwenyekiti wa
Taifa ,Mheshimiwa Jakaya Kikwete inathamini sana imani ya wanachama
wa Diaspora na kazi wanayofanya kukiimarisha Chama Cha Mapinduzi.
Mh. January Makamba aliahidi wana Diaspora kuwa Chama Cha Mapinduzi
kinaweka mfumo mzuri ili kuyatumia mawazo ya wana CCM walioko nje ya
Nchi ili kukiimarisha Chama.
Shina Jipya la CCM Leicester
1. Cletus Shigela – Mwenyekiti
2. Moses Kusamba – Katibu
3. Hussein Hussein – Mjumbe
4. Pauline Nzengula – Mjumbe
5. Agness J Nyehunge - Mjumbe
6. Mzee Khalid Kassim Ndagiye (Mlezi)
Katika ufunguzi huo ambao ulihudhuliwa na wana Leicester wengi , hoja
mbalimbali katika masuala ya kukiendeleza chama katika utawala wa nchi
zilijadiliwa na kutolewa ufafanuzi na viongozi wa Tawi akiwemo Mh. Haruna
Mbeyu “Special Advisor”, Bw. John Lyimo - Uchumi na Fedha, Bw. Abraham
Sangiwa Naibu Katibu Uenezi na Siasa Tawi na Bw. Albert Ntemi Naibu
Katibu Tawi.
Baada ya mahojiano na Uongozi wa Tawi na kujibu maswali yaliyokuwa
yakiwasumbua wanachama, wakereketwa na makada wengi , wanachama
wapya wengi walijitokeza na kujiunga na CCM papohapo na kukabidhiwa
Kadi za uanachama na Katibu wa Tawi Bi. Mungula,huku wakishangiliwa
na kupongezwa na wanachama wenzao na uongozi mpya wa Tawi la CCM
UK. Waliobaki katika wahudhuriaji hao walishakuwa na kadi za Chama Cha
Mapinduzi zamani na hivyo walionyesha furaha kubwa kuwa sasa wataweza
kuzitumia kadi zao baada ya kuwa na Shina katika mji wao.
Kabla ya uchaguzi wa viongozi wa shina jipya ambao uliendeshwa kwa
demokrasia ya hali ya juu, akijibu hoja za wana Leicester Naibu Katibu wa
Siasa na Uenezi wa Tawi Bw. Abraham Sangiwa aliwakumbusha wajumbe
kuzifahamu haki, sifa na wajibu wa uanachama na miiko ya uongozi kama
ilivyoainishwa katika miongozo na Katiba ya Chama Cha Mapinduzi.
Kidumu Chama Cha Mapinduzi
Mariam Mungula
Katibu wa Tawi la Chama Cha Mapinduzi, Uingereza
CHAMA CHA MAPINDUZI -UK.
Imetolewa na Idara ya Siasa na Uenezi, Tawi la CCM ,Uingereza.
Tarehe: 10 Septemba 2012.
No comments:
Post a Comment