TPBC Yaipa Shavu BFT - Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari
TAARIFA KW A VYOMBO VYA HABARI
Kamisheni
ya Ngumi za Kulipwa Nchini (TPBC) inaipa shavu BFT kwa juhudi zake za
kuendeleza ngumi za ridhaa hapa nchini kama kichocheo cha maendeleo ya
ngumi pamoja na michezo yote kwa ujumla.
TPBC
inatambua ugumu wa maisha pamoja na matatizo yaliyopo kupata wadhamini
kwenye mchezo wa ngumi. Juhudi za BFT za kuandaa mashindano ya nguni za
ridhaa mwaka huu ni zenye mweleko mzuri kimaendeleo. Sisi kama Kamisheni
iliyopewa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jukumu la
kusimamia ngumi za kulipwa nchini tunatambua kuwa ngumi za ridhaa ni
chemchem ya nguni za kulipwa hivyo tupo tayari kushirikiana na BFT
kufanikisha mashindandano haya.
TPBC
imefarijika na juhudi za BFT katika ushiriki wake kwenye mashindano ya
Olympic yaliyomalizika hivi karibuni nchini Uingereza. Juhudi zenu
zimeitangaza vyema Tanzania na kuwapatia mabondia wa Kitanzania nafasi
ya kujulikana ulimwenguni.
Kushiriki
katika mashindano ya Olympic sio tu kupata medali bali pia ushiriki
wenyewe unaitangaza nchi kama moja ya mataifa yaliyo mstari wa mbele
katika maendeleo ya michezo ulimwenguni.
Tunatoa
pia pongezi kwa Kamati ya Olympic ya taifa (TOC) na baraza la Michezo
la taifa (BMT) kwa juhudi zake za kuhakikisha kuwa kila mara Tanzania
inakuwa moja ya nchi zinazoshiriki katika mashindano ya Olympic.
Sisi
tunashiriki katika mapambano mbalimbali ya ngumi za kulipwa ulimwenguni
tunajua faida za kujitangaza huku kwani tunajulikana kwa juhudi hizi.
Tutatoa wito kwa wadau wa ngumi na michezo yote Tanzania ikiwa ni pamoja
na watu binafsi, makampuni mbalimbali pamoja na na taasisi zisizo za
kiserikali kuwasidiaBFT katika juhudi za kuendesha mashindano haya
yatakayoanza hivi karibuni.
Imetolewa na:
Onesmo Ngowi
Rais wa Kamisheni ay Nguni za Kulipwa Nchini (TPBC)
Mkurugenzi wa Ngumi wa Jukuiyaya madolka (CBC)
Rais wa Shirikisho la Ngumi la Kimataifa Afrika, Ghuba ya Uarabu na Uajemi
No comments:
Post a Comment