Athari za kimbunga Sandy mjini New York
Mojawapo
ya vimbunga vikubwa zaidi kuwahi kupiga Mashariki mwa Pwani ya Marekani
kimesababisha mafuriko makubwa katika baadhi ya sehemu za mji wa New
York.
Maeneo mengi mjini yamewachwa katika giza baada ya huduma za umeme kukatizwa.
Kimbunga hicho kilipiga ardhi kwenye Pwani ya New Jersey karibu na mji wa Atalanta muda mfupi jana usiku/
Dhoruba kali kutoka mjini Florida hadi nchini
Canada imepiga Mashariki mwa Marekani na kusababisha mawimbi makali
mjini New York.
Maji yamefurika kwenye barabara na katika njia
za reli pamoja, maeneo ya kuegesha magari na katika eneo la Ground Zero,
eneo ambalo mashambulizi ya Septemba kumi na moja yalitokea.
Sehemu kubwa za mji wa New York ziko kwenye giza baada ya milingoti ya umeme kuharibiwa.
Wagonjwa waliondolewa kwenye hospitali moja baada ya umeme kukatika.
Zaidi ya watu milioni tano walisemekana kukosa
umeme katika eneo la Pwani baada dhoruba kali huku takriban wengine
milioni moja wakishauriwa kuhama nyumba zao. Athari za kimbunga hicho
labda huenda zikajulikana baadaye leo.
No comments:
Post a Comment