Meli za Iran ilitia nanga katika badnari ya Sudan.
Msururu
mdogo wa meli za jeshi la wanamaji la Iran umetia nanga katika bandari
ya Sudan kuwasilisha kile ambacho shirika la kitaifa la habari Iran ISNA
linasema ni ujumbe wa amani na usalama.
Ziara hiyo katika bandari ya Sudan inajiri siku
sita baada ya shambulio la angani dhidi ya kiwanda cha silaha mjini
Khartoum ambalo serikali nchini humo imeilaumu Israeli kulitekeleza.
Sudan imelalamikia Umoja wa Mataifa kuwa Israel ilishambulia kiwanda chake ambacho kinaaminiwa kuendeshwa na Iran.
Hata hivyo, Israel haijathibitisha au kukana ikiwa ndiyo ilihusika na shambulio hilo.
Kulingana na shirika la habari la serikali, meli
hizo zilizowasili nchini Sudan Jumatatu asubuhi, inajumuisha meli
inayoweza kubeba helikopta tatu.
Ziara ya meli ya kivita za Iran nchini Sudan, ni ishara kuwa uhusiano wa kiusalama kati ya nchi hizo mbili.
Kiwanda cha silaha ambacho kililengwa kwa
mashambulizi hayo, inaaminiwa na wadadisi kuwa kiwanda cha Iran
kinachotengeza silaha na zana zengine za kivita baadhi ambazo huingizwa
kimagendo nchini Misri kuwaendea wapiganaji wa Hamas katika ukanda wa
Gaza.
Israel imekataa kutoa tamko lolote kuhusu shambulizi hilo
No comments:
Post a Comment