Takriban watu
arobaini na moja wameuawa na wengine arobaini kujeruhiwa katika
shambulizi la bomu lililotokea nje ya msikiti katika eneo la Maymana.
Shambulio hilo lilitekelezwa nje ya msikiti waumini walipokuwa wakishereheka siku kuu ya Eid al-Adha.
Afisaa mmoja katika mkoa huo alisema
kuwa gavana wa eneo hilo pamoja na mkuu wa polisi walikuwa ndani ya
smikiti huo wakati wa shambulizi.
Alisema kuwa maafisa wa serikali hawakujeruhiwa lakini polisi na wanajeshi ni miongoni mwa waliojeruhiwa.
Walioshuhudia walisema kuwa mtu huyo wa
kujitolea mhanga alikaribia msikiti na kutegua mabomu aliyokuwa
amefungiwa kifuani baada ya sala ya Eid kukamilika, na waumini kusimama
nje ya msikiti wakijuliana hali.
Haijulikani jinsi mtu huyo alivyoweza kupita
vizuizi vinne kabla ya kufikia msikiti huo. Vizuizi hivyo vya usalama
viliwekwa kwa sababu watu wanahofia kushambuliwa wakati huu wa sikukuu.
Afisa mmoja wa usalama alieleza kuwa
mshambuliaji huyo alikuwa amevalia sare za polisi, ambazo huenda
ziliwapumbaza maafisa wa usalama katika vizuizi hivyo.
Gavana wa Mkoa, wanasiasa wa vyeo vya juu na mkuu wa polisi walikuwa miongoni mwa wale waliokuwa wakishiriki sala hiyo Shambulio
hilo limetokea siku chache tu baada ya kundi la wapiganaji kuwaua
maafisa kadhaa wa Serikali katika Mkoa huo, kukiwemo aliyekuwa wakati
mmoja afisa mkuu wa Taliban ambaye baadaye alijiunga na Serikali katika
eneo la Faryab.
Usalama umedumishwa kote nchini Afghanistan wakati huu wa siku kuu ya Eid.
No comments:
Post a Comment