Meli Ya Utoaji Mimba Yazuiliwa Kuingia Morocco
Meli
moja ya Uholanzi iliyokuwa ikielekea katika pwani ya Morocco kutoa
huduma ya utoaji mimba kwa wanawake imezuiliwa kuingia bandarani kwa
mujibu wa wanaharakati walioituma nchini humo.
Kundi
la wanaharakati hao wanawake linasema kuwa bandari ya Smir imefungwa
kabisa na meli za kivita zinalinda doria eneo la bandari hiyo.
Hapo
jana Morocco ilisema kuwa meli hiyo haijapewa mualiko na mamlaka
zinazotambuliwa nchini humo na hivyo ilikuwa ikifanya shughuli hiyo
kinyume cha sheria.
Sheria za Morocco zinakataza utoaji mimba isipokuwa tu iwapo maisha ya
mwanamke mjamzito yako hatarini.
Ibtissame
Lachgar, ambaye ni mmoja wa wanaharakati wanaotetea haki ya utoaji
mimba amesema wanawake wengi wanalazimika kufanya utoaji mimba kwa njia
zisizo rasmi ambazo ni hatari.
No comments:
Post a Comment