Mazishi ya Papa Shenouda yalifanyika mapema mwaka huu
Baraza la maaskofu wa Kikopti nchini Misri, linatarajiwa kumpigia kura mrithi wa papa Shenouda wa tatu aliyefariki mwezi Machi.
Maaskofu wawili na watawa watatu wako kwenye
orodha ya wale wanaogombea wadhifa huo ambapo yeyote atakayeshinda
atakuwa kiongozi wa miamoja na kumi na nane kuongoza madheheyo hayo
ambayo ndio kundi ndogo sana la wakristo duniani.
Baraza hilo litachagua wagombea
watatu na kuandika majina yao kwenye vijikaratasi ambavyo vitawekwa
kwenye boxi katika mimbar ya kanisa la mtakakatifu Mark, mjini Cairo.
Kisha mtoto atakayekuwa amefumbwa macho,
atachukua kijikaratasi kimoja kutoka kwenye boxi hilo, jina la atakekuwa
amechukua ndiye atakuwa Papa mpya.
Atayakuchaguliwa ataapishwa katika sherehe itakayofanyika tarehe 19 mwezi Novemba.
Papa Shenouda wa tatu aliongoza waumini wa
kanisa hilo nchini Misri kwa miongo minne na alifariki akiwa na umri wa
miaka 88 mwezi Machi, baada ya kuugua saratani.
Aliwataka maafisa wa kanisa hilo kufanya kila
wawezalo kushughulikia maswala muhimu ya waumini wa kanisa hilo baada ya
mashambulizi kadhaa dhidi ya makanisa katika miaka ya hivi karibuni.
Mrithi wake anakabiliwa na kibarua cha
kuwahakikishia kuimarika kwa imani jamii ya waumini wa kanisa hilo hasa
wakati huu ambapo harakati za makundi ya kiisilamu zimeshika kasi nchini
Misri.
Vijana wengi wa kikopti watakuwa wanatazamia
kupata kiongozi atakayewasaidia kuweka bayana majukumu yao chini ya
utawala usio kuwa wa Mubarak.
No comments:
Post a Comment