Mamia ya wachimba migodi wamekataa kurejea kazini na hivyo kufutwa kazi
Zaidi ya wachimba
migodi 8,000 waliokuwa wanagoma , nchini Afrika Kusini, wamefutwa kazi
baada ya kukataa kurejea kazini.
Wamiliki wa mgodi wa Gold Fields wamesema kuwa
wafanyakazi hao walipuuza makataa ya jana saa kumi jioni kurejea kazini
ndipo wakafutwa kazi
Wiki jana takriban wachimba migodi 11,000 wa kampuni ya madini ya Gold Fields, walitii agizo la kampuni kurejea kazini .
Sekta ya mdini nchini Afrika Kusini ilikumwba na migomo pamoja na vurugu na kusababisha vifo vya watu hamisni.
Wafanyakazi wamekuwa wakidai nyongeza ya
mishahara na mazingira bora ya kazi ingawa hatua iliyochukuliwa kuhusu
mgodi wa KDC East, Magharibi mwa Johannesburg -inahusiana na vyama vya
wafanyakazi wala sio mishahara.
"wafanyakazi wote 8,500 waliokuwa wamegoma, hawakurejea kazini '' alisema msemaji wa kampuni hiyo, Sven Lunsche.
"Hawakurejea kazini kwa hivyo tumewapa wote
barua za kuwaachisha kazi.'' Aliongeza kuwa wafanyakazi hao wana siku
moja kukata rufaa
"sasa tumefika sehemu ambapo hatuwezi kuwa
wavumilivu tena . Tumelazimika kuchukua hatua na tumefanya hivyo, "
alisema bwana Lunsche.
"tunachunguza hali na tuna polisi walio tayari kuchukua hatua ikiwa vurugu litatokea. Lakini kufikia sasa mambo yako shwari.''
Kampuni ya Gold Fields ilitoa onyo la mwisho kwa
wafanyakazi kwenda kazini kuanzia Jumatatu tarehe 22 mwezi huu au
wachukuliwe hatua.
Kampuni hiyo ilipata kibali kutoka kwa mahakama kutaja mgomo wao haramu.
Migomo katika sekta ya madini nchini Afrika Kusini imeathiri sana uchumi wa nchi hiyo huku sarafu ya nchi ikipoteza thamani.
No comments:
Post a Comment