Wapiganaji Mali wanunua watoto jeshini
Wapiganaji wa Tuareg
Wapiganaji wa
kiisilamu wanaodhibiti sehemu za Kaskazini mwa Mali, wanajipatia pesa
kutoka kwa biashara haramu ya mihadarati na kupitia kwa visa vya utekaji
nyara ambapo wanalipwa kikombozi ili kuwaachilia mateka.
wakati wakitumia sheria ya kiisilamu katika maeneo wanayodhibiti.
Madai haya ni kwa mujibu wa afisaa mmoja mkuu wa Umoja wa Mataifa.
Wapiganaji hao pia wananunua watoto kuwatumia
kama wanajeshi, huku wakilipa familia za watoto hao dola mia sita kwa
kila mtoto. Alisema Ivan Simonovic baada ya kuzuru nchi hiyo.
Wapiganaji hao wenye siasa kali, walitwaa
thuluthi mbili za udhibiti wa Mali, wakati nchi hiyo ilipotumbukia
katika vita baada ya kufanyika mapinduzi ya kijeshi.
Bwana Simonovic alitoa picha ya kutisha kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanyika katika eneo hilo.
''Haki za wanawake hasa zinakiukwa pakubwa''
alisema afisaa huyo ambaye ni naibu wa katibu mkuu kuhusu haki za
binadamu katika Umoja wa mataifa ,akielezea kuhusu orodha ya wanawake
ambao hawajaolewa au wale ambao walikuwa wamepata watoto.
Wanawake zaidi wanalazimishwa kuolewa huku gharama ya kupata mke ikiwa dola elfu moja.
''Visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu hapa ni
vya kushtua na vinafanyika sana'' aliambia waandishi wa habari mjini
New York, akiongeza kuwa wapiganaji hao wanatumia sheria kali za
kiisilamu kudhibiti eneo hilo.
Katika ziara ya afisaa huyo ambayo ilinuia
kugundua yanayoendelea nchini Mali, aligundua kuwa wapiganaji hao
wanatumia sheria kali kwa wahalifu.
Hadi kufikia sasa, watu watatu wamenyongwa hadharani na wengine wanane kukatwa mikono huku wawili wakichapwa hadharani.
No comments:
Post a Comment