Ban Ki-moon alaani mashambulizi Gaza


Mashambulizi yasababisha hasara kubwa
Mashambulizi yasababisha hasara kubwa

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa ametoa wito kwa Israel kukomesha mara moja mashumbulizi yake dhidi ya Gaza, huku mashambulizi hayo yakiendelea kwa siku ya sita mfululizo.

Ban Ki-moon alisema kwamba anaelekea mjini Cairo ili kujiunga na mazumgumzo yatakayojadili vile mapigano hayo yanaweza kusitishwa angalau kwa muda.

Mashumbulizi ya Israel, chini ya mkakati Operation Pillar of Defence, Jumapili ndiyo yalikuwa makali zaidi tangu yaanze, huku Israel ikisema kwamba ilikuwa inalenga makaazi ya wanamgambo wa Hamas.

Wapalestinina 80 na Waisraeli watatu wameuawawa katika siku hizi sita, duru rasmi zimesema, huku Israel ikizidi kuishambulia Gaza kutoka baharini na angani, na kwa upande wao wanamgambo wa Hamas wakizidi kurusha makombora.

Jumapili, Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu alisema kwamba alikuwa tayari kuendelea na mashambulizi hayo, baada ya Israel kuidhinisha wanajeshi zaidi wa akiba 75,000.

Ingawaje Misri inajitahidi kuongoza majadiliano kusitisha mapigano hayo, na kiongozi wa ngazi ya juu wa Israel ameshawasili Cairo, idadi ya vifo ingali inazidi kuongezeka.

Mashambulizi dhidi ya Gaza yaliendelea mapema Jumatatu, huku shambulizi moja likiangamiza kituo kimoja cha polisi cha Hamas.

No comments:

Post a Comment