Rais wa Nigeria ameonya kuwa
matokeo yanaweza kuwa mabaya kwa Afrika iwapo wapiganaji wa Kiislamu
hawataondoshwa kaskazini mwa Mali.
Rais Goodluck Jonathan alisema Nigeria inataka kikosi cha jeshi kipelekwe huko haraka.
Alisema wapiganaji wamelifanya eneo kubwa la Mali kuwa halina sheria.
Rais Jonathan alisema hayo kwenye mkutano wa
viongozi wa Afrika magharibi wa jumuia ya ECOWAS mjini Abuja, ambako
wanajadili mpango wa kutuma wanajeshi elfu kadha Mali iwapo majadiliano
na wapiganaji hayatafanikiwa.
Umoja wa Mataifa umetoa idhini kuingilia kati kijeshi nchini Mali.
No comments:
Post a Comment