Mirungi yamfikisha kortini


Dawa za kulevya aina ya Mirungi.

Mchukuzi Seleman Said (20), Mkazi wa Mbagala Kongowe Mzinga, Wilaya ya Temeke,  amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Wilaya ya Ilala kwa kukabiliwa na shitaka la kukutwa na dawa za kulevya aina ya Mirungi.

Wakili wa Serikali, Anuciatha Leopard, alidai mbele ya Hakimu Tarsila Kisoka kuwa Julai 17, mwaka huu, katika maeneo ya Mamlaka ya Bandari ya Dar es Salaam, alikutwa na dawa hizo paketi tatu.

Mshitakiwa alikana shitaka hilo na yupo rumande kutokana na kushindwa kutimiza masharti ya dhamana. Hakimu Kisoka aliahirisha shauri hilo mpaka Novemba 22, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa tena.

Wakati huo huo, Ramadhani Suleiman (35) amefikishwa katika Mahakama ya Mwanzo ya Kariakoo kujibu shitala la kutishia kuua kwa kutumia silaha.

Karani Lucy Luta, alimsomea shitaka mtuhumiwa huyo mbele ya Hakimu Christina Luguru, kuwa Oktoba 22, mwaka huu, maeneo ya Mchikichini, mshitakiwa huyo alimtishia kumuua mlalamikaji Mariamu Iddy kwa kutumia panga.

Mtuhumiwa huyo alikana shitaka hilo na yupo rumande kwa kukosa dhamana. Hakimu Luguru alihirisha kesi hiyo mpaka Novemba 22, mwaka huu kwa ajili ya kusikilizwa tena.

No comments:

Post a Comment