Mkewe Gbagbo kufikishwa the Haque
Simone Gbagbo
Mahakama ya kimataifa ya Jinai
ICC, imetoa kibali cha kukamatwa kwa mke wa aliyekuwa rais wa Ivory
Coast Laurent Gbagbo, Bi Simone, Gbagbo.
Bi Gbagbo anasakwa kwa tuhuma za kuhusika na
uhalifu wa kivita wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoibuka
baada ya uchaguzi wa urais nchini humo.
Mumewe
tayari amekamatwa na anasubiri kesi yake kuanza katika mahakama hiyo
iliyoko The Haque, kuhusiana na madai hayo ya uhalifu wa kivita.
Takriban watu 3,000 waliuawa kwenye machafuko yaliyotokea baada ya ya Gbagbo kukataa kukubali matokeo ya uchaguzi wa Urais.
Gbagbo na mkewe walikamatwa ndani ya handaki moja Aprili mwaka wa 2011, miezi mitano, baada ya uchaguzi wa urais.
Wanajeshi wa rais wa sasa wakiungwa mkono na
wanajeshi wa Umoja wa Mataifa walianzisha msako mkali dhidi yao, baada
ya kujificha ndani ya ikulu ya rais.
anatuhumiwa kuhusika na mauaji, ubakaji, dhuluma
na ngona na kuwadhulumu wapinzani wa serikali miongoni mwa mashtaka
mengine mjini Abidjan.
Licha ya kuwa Bi Gbagbo hakuwa akiwania kiti
chochote cha kisiasa, ripoti zinasema kuwa alikuwa na mamlaka makubwa na
kuwa alimshawishi mumeo kutokubali matokeo ya uchaguzi.
Gbagbo, 67, alihamishwa hadi The Haque mwaka
uliopita, na kuandikisha historia ya kuwa rais anayeondoka wa kwanza
kufikishwa mbele ya mahakama hiyo ya ICC.
Rais huyo wa zamani amekanusha madai hayo yote.
Kabla ya kuhamishwa hadi the Haque, Gbagbo na
mkewe mwenye umri wa miaka 63, walifunguliwa mashtaka nchini Ivory Coast
kuhusiana na uhalifu wa kiuchumi, ikiwemo mdai ya kupora mali, wizi wa
nguvu na kutumia rasilimali za umma kwa njia mbaya
Mahakama hiyo ya ICC sasa imetoa wito kwa
serikali ya Ivory Coast, kumusafirisha Bi Gbagbo ili afunguliwa mashtaka
huko the Haque.
No comments:
Post a Comment