Mkuu wa Majeshi DRC afutwa kazi
Generali Amisi
Mkuu wa majeshi nchini Jamuhuri
ya Kidemokrasia ya Congo, amesimamishwa kazi huku uchunguzi ukiendelea
kufuatia madai kuwa aliwauzia silaha makundi ya waasi yanaopambana na
serikali ya nchi hiyo.
Ripoti moja ya Umoja wa Mataifa, imemtuhumu,
Generali Gabriel Amisi kwa kuendesha mtandao wa kusambaza silaha kwa
wawindaji haramu na makundi ya waasi, likiwemo kundi la Mai Mai Raia
Mutomboki.
Msemaji wa serikali ya nchi hiyo amesema, maafisa kadhaa wa jeshi pia wanachunguzwa.
Serikali ya Rais Kabila imemfuta kazi mkuu huyo
wa majeshi, siku chache baada ya waasi wa M23 kuuteka mji wa Goma
Mashariki mwa nchi hiyo.
Waasi hao mpia wameutekja mji wa Sake, lakini
msemaji wa serikali Lambert Mende, amesema wanajeshi wa serikali
wamefanikiwa kuumboa tena mji huo mdogo.
Waasi hao ambao wanaaminika kuungwa mkono na
serikali za Rwanda na Uganda, wametishia kuendeleza mapigano hayo hadi
mji mkuu wa Kinshasa, ikiwa rais Joseph Kabila hatabuli kuanzisha
mazungumzo ya amani.
Mazungumzo ya Amani
Uganda inaandaa mkutano wa marais wa Rwanda na
Uganda hii leo na kuna ripoti kuwa baadhi ya viongozi wa kundi hilo la
waasi wa M23 wamesafiri mjini Kampala kushiriki katika mazungumzo hayo.
Ripoti iliyoandikiwa Umoja wa Mataifa na kundi
moja wa wataalamu huru, imesema kuwa Generali Amisi, anaendesha mtandao
wa kusambaza silaha kwa makundi ya kihalifu na waasi wanaohudumu
Mashariki mwa Congo, eneo ambao bado kuna idadi kubwa ya wapiganaji wa
waasi.
Hata hivyo kundi hilo la M23 halikuwa miongoni
mwa makundi yaliyotajwa kwenye ripoti hiyo lakini kundi la Raia
Mutomboki, moja ya makundi kadhaa yanayojumuisha wapiganaji wa Mai Mai,
inaaminika kuwa na uhusiano wa karibu na kundi hilo la M23.
Ripoti hiyo ya Umoja wa Mataifa imenadi kuwa
Generali Amisi aliagiza bundi 300, aina ya AK-47 kukabithiwa kundi moja
linalohudumu katika eneo hilo la mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia
ya Congo, lijulikanalo kama Nyatura.
Ripoti hiyo imeongeza kusema kuwa waasi hao
wananunua risasi kutoka kwa nchi jirani ya Congo na kusafirisha kupitia
Kinshasa hado Mashariki mwa nchi hiyo na mtandao unaoendeshwa na
washirika wa Generali Amisi, wakiwemo baadhi ya jamaa ya familia yake.
No comments:
Post a Comment