Afisa mmoja mkuu wa usalama nchini Libya amepigwa risasi na kuuawa nje ya nyumba yake mjini Benghazi.
Wizara ya usalama wa ndani nchini humo imeelezea
kuwa Bwana Farraj al-Dursi , ambaye alikuwa mkuu wa polisi mjini humo,
amefariki kutokana na majeraha ya risasi baada ya kushambuliwa na watu
wasiojulikana.
Kumekuwa na visa vingi vya mauji mjini Benghazi katika siku za hivi punde.
Mnamo mwezi Septemba, balozi wa marekani mjini Benghazi aliuawa pamoja na wamarekani watatu katika ubalozi huo.
Col Dursia aliteuliwa kuwa mku wa polisi mjini
humo muda mfupi baada ya shambulio lililotekelezwa kwenye ubalozi wa
Marekani, ambalo balozi wa Marekani na maafisa watatu waliuawa.
Maafisa kadhaa wa Ulinzi wameuawa na watu
wasiojulikana mjini Benghazi, mji ambao maandamano na machafuko
yaliyomuondoa madarakani Muamarr Gaddafi yalianza.
Mwandishi wa BBC mjini Tripoli, anasema wengi wa
maafisa hao wanalengwa kwa sababu wanakisiwa kuwa na uhusiano na
serikali ya ya zamani ya nchi hiyo.
Kabla ya serikali, ya Gadaffi kuondolewa
madarakani, Kanali, Dursi alifahamika kuwa afisa aliyehusika na kitengo
cha kupambana na dawa za kulevya.
No comments:
Post a Comment