Waasi wa M23
Waasi nchini Jamuhuri ya Kidemokrasi ay Congo, wamepuuzilia mbali wito kutoka kwa viongozi wa kimataifa wa kusitisha mapigano na pia kuondoka kutoka mji wa Goma Mashariki mwa nchi hiyo.
Msemaji wa kundi hilo la waasi wa M23, amesema wapiganaji wao wataendelea na mapigano hayo hadi pale serikali ya rais Joseph Kabila itakapokubali kutekeleza masharti yao.
Awali rais wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, alisema yuko tayari kuchunguza malalamishi ya wapiganaji wa waasi ambao wameuteka mji wa Goma, Mashariki mwa nchi hiyo.
Akiongea baada ya mazungumzo yaliyofanyika nchini Uganda na Kuhudhuriwa na rais wa Rwanda, Paul Kagame, Rais Joseph Kabila amesema anatathmini uwezekano wa kuanzisha mazungumzo na waasi hao wa M23.
Mwenyekiti na mwenyeji wa Mazungumzo hayo, rais wa Uganda Yoweri Museveni, rais Kabila na Kagame kwa kauili moja walitoa wito wa kusitishwa kwa mapigano hayo na pia kutoa amri kwa waasi hao kuondoka Goma mara moja.
Wapiganji hao wa waasi wametishia kuendeleza mapigano hayo hadi mji mkuu wa nchi hiyo Kinshasa.
Mazungumzo ya amani
Wanajeshi wa Serikali ya Congo
No comments:
Post a Comment