Uingereza yatoa ilani ya ugaidi Misri

Wizara ya Mashauri ya Nchi za Nje ya Uingereza imeonya kwamba uwezekano unazidi kwamba kutatokea mashambulio ya kigaidi katika eneo la Sinai nchini Misri; na imezidisha uzito wa onyo hilo kutoka la kawaida na kuwa kubwa zaidi.

Magari ya jeshi la Misri katika eneo la Sinai

Ilani hiyo imetolewa kutokana na taarifa za hivi karibuni kuhusu ile inayosemekana kuwa njama ya al-Qaeda na kupatikana kwa silaha katika eneo hilo la Sinai.

Piya linafuata polisi wa Misri kugundua kikundi cha magaidi mjini Cairo, na baadhi ya taarifa zinaeleza magaidi hao wakipanga kushambulia watalii kutoka mataifa ya Magharibi.

Hata hivyo Wizara ya Mashauri ya Nchi za Nje ya Uingereza inasema hali katika maeneo ya watalii ya Bahari ya Sham, pamoja na Sharm el Sheikh, ni tulivu.

No comments:

Post a Comment