Wapiganaji wa waasi wa M23,
hatimaye wamefanikiwa kuingia mji mkuu wa eneo la Mashariki mwa Jamuhuri
ya Kidemokrasia ya Congo, eneo lenye utajiri mkubwa wa madini.
Mwandishi wa BBC mjini Goma anasema wapiganaji
hao wa waasi walikabiliana kwa risasi na wanajeshi wa serikali, ambao
walitoroka baada ya kuzidiwa nguvu.
Jeshi
la Umoja wa Matifa la Kutunza amani katika eneo hilo limekanusha madai
kuwa wapiganaji hao wa waasi wanathibiti uwanja wa NDEGE.
Maelfu ya watu wametoroka makwao kufuatia
mapigano hayo, ambayo yamezua wasi wasi wa kuzuka upya kwa mapigano
nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, mapigano ambayo yamesababisha
vifo vya takriban watu milioni tano.
Hii ni mara ya kwanza tangu kumalizika kwa
mapigano mwaka wa 2003, ambapo wanajeshi wa waasi wamefanikiwa kuingia
mji huo wa Goma. Takriban watu nusu milioni wanakadiriwa wanaishi mjini humo.
Serikali ya Rwanda imekanusha madai ya mara kwa
mara kutoka kwa serikali ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuwa
inawaunga mkono wapiganaji hao wa waasi wa M23.
Awali serikali ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya
Congo, ilipuuzilia mbali makataa iliyotolewa na wapiganaji wa waasi wa
kuanzisha mazungumzo ya amani, na kukariri kuwa itaendelea kuilinbda mji
wa Goma, Mashariki mwa nchi hiyo.
Baraza la usalama la umoja wa mataifa umelaaini hatua hiyo ya waasi wa M23 ya kuendelea na mapigano huku wakielekea mji wa Goma.
Mapigano hayo yametajwa kuwa mabaya zaidi tangu mwezi Julai Mwaka huu katika eneo hilo lenye utajiri mkubwa wa madini.
No comments:
Post a Comment