Wapigani wa waasi nchini jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wametishia kuendeleza mapigano hadi mji mkuu wa nchi hiyo Kinshasa, siku chache tu baada ya kuuteka mji wa Goma.
Msemaji wa kundi hilo la waasi wa M23 rLt Col Vianney Kazarama amewaambia watu waliokuwa wamekusanyika mjini Goma kuwa wako tayari kukomba taifa hilo.
Awali Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha kwa kauli moja azimio linalolaani kutekwa kwa mji wa Goma nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na waasi wa M23.
Azimio hilo pia linamtaka katibu mkuu wa Umoja huo kuripoti kuhusu madai ya uungwaji mkono wa mataifa ya kigeni kwa makundi ya uasi yaliyoanza harakati zao nchini Congo miezi minane iliyopita.
Baraza la usalam la Umoja wa mataifa limelaani vikali kitendo cha waasi wa M23 wa cha kuuteka mji wa Goma.
Baraza la usalama la Umoja wa mataifa tayari limeidhinisha vikwazo dhidi ya mkuu wa kundi hilo na limesema limenuia vikwazo hivyo vitawalenga viongozi zaidi wa waasi .
Wajumbe wa baraza hilo wameelezea hofu kubwa juu ya shutuma kuwa waasi hao wanaungwa mkono kutoka nje hatua iliyopelekea waasi wa M23 kuwa na uwezo mkubwa zaidi wa kijeshi
Katibu mkuu wa UN kuchunguza madai
Baraza hilo limemtaka katibu mkuu wa Umoja huo kuchunguza ripoti kuhusiana na shutuma hizo.
No comments:
Post a Comment