Wabunge Somalia waidhinisha mawaziri
Wabunge wa Somalia
Bunge nchini Somalia
limeidhinisha baraza jipya la mawaziri kumi waliloteuliwa na waziri mkuu
Abdi Farah Shirdon. Wanawake wawili ni miongoni mwa walioteuliwa.
Serikali kwa mara ya kwanza ina waziri wa kwanza
mwanamke atakayeshikilia wadhifa wa waziri wa mambo ya nje, Fauzia
Yusuf Haji Adan na ambaye anatoka Somaliland.
Kuidhinishwa kwa baraza hilo
kumekuja licha ya ripoti kuwa baadhi ya koo hazikuwakilishwa vyema
kwenye baraza hilo liliotajwa wiki moja iliyopita.
"Wabunge walipitisha baraza hilo kwa kura 219 ,
kati ya wabunge 225, waliohuduhuria kikao'' alisema spika wa bunge
Mohamed Osman Jawari.
Wabunge watatu waliwakataa mawaziri hao huku wengine watatu wakijizuia kupiga kura.''
Rais mpya pamoja na wabunge wapya walichaguliwa
hivi karibuni nchini Somalia , nchi iliyokuwa haina serikali thabiti kwa
zaidi ya miaka 20.
Serikali mpya inakabiliwa na changamoto nyingi
wakati ikijaribu kuleta utulivu na utahbiti katika nchi hiyo ambayo
imekumbwa na vita vya muda mrefu pamoja na tisho la wanamgambo wa Al
Shabaab ambao wametishia kuipindua wakisema inaungwa mkono na nchi za
Magharibi.
No comments:
Post a Comment