Wasi wasi kuhusu virusi vya Ebola


Nguruwe
Nguruwe

Utafiti wa wanasayansi kutoka Canada unaashiria kuwa aina hatari zaidi ya virusi vya Ebola inaweza kusambazwa hewani kati ya aina mbili ya viumbe.

Matokeo ya utafiti huo, yanasema kuwa nguruwe waliokuwa wameambukizwa aina ya Ebola kutoka Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, waliweza kuipitisha kwa nyani, bila ya kugusana.

Watafiti hao wanadhani maambukizi ya aina hiyo yanachangia kusambaa kwa ugonjwa huo hatari barani Afrika, na kwamba nguruwe huenda wanabeba virusi hivyo.

Lakini wanaamini ugonjwa huo unaweza tu kusambazwa katika eneo dogo, na hauwezi kusambaa haraka kama homa.

Nchini Uganda, mkurupuko mpya wa Ebola umewauawa watu wawili karibu na mji mkuu, Kampala.

Virusi vya ugonjwa huop wa Ebola, husababisha maafa kwa bvinadamu na viumbe vingine mbali na binadamu.

Matokeo ya uchunguzi huo yamechapishwa kwenye jarida ya kimatibabu.

Kwa mujibu wa Shirika la afya duniani WHO, maambukizi miongoni mwa binadamu husambazwa kwa watu kukaribiana, kupitia damu, unyevu mwilini na maji maji yanayotokana na wanyama wengine kama vile, sokwe na Swara.

Popo vile vile amekisiwa kuwa chanzo cha maambukizi hayo ya viruso vya ebola.
Lakini baada ya utafiti kufanya, imebainika kuwa nguruwe wanaofugwa nyumbani au wale wa mwituni wanaweza kuwa vyanzo vya virusi hivyo ambavyo ni hatari zaidi.

No comments:

Post a Comment