Zuma amtembelea Mandela hospitali
Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, amemtembelea rais wa zamani, Nelson Mandela, hospitali mjini Pretoria.
Rais Zuma alisema Bwana Mandela akionesha katika hali nzuri baada ya kupumzika usiku kucha.
Hapo awali wakuu wa serikali walisema Bwana
Mandela alilazwa hospitali Jumamosi kwa ukaguzi, na kwamba hali ya mzee
huyo wa miaka 94 siyo ya kutia wasiwasi.
Bwana Mandela alilazwa hospitali mwezi wa Februari kutibiwa matatizo ya tumbo aliyokuwa nayo kwa muda mrefu.
Hakuonekana hadharani tangu Afrika Kusini ilipofungua michezo ya Kombe la Dunia mwaka wa 2010.
No comments:
Post a Comment