David Cecil akiwa korokoroni
Mahakama moja nchini Uganda, imefutilia mbali kesi dhidi ya mwandishi mmoja wa michezo ya tamthilia, David Cecil, ambaye alikuwa akikabiliwa na shitaka la kuonyesha mchezo kuhusu hali ya wapenzi wa jinsia moja, katika mji mkuu wa nchi hiyo Kampala.
Bwana Cecil, alikabiliwa na tuhuma za kukiuka sheria kwa makusudi.
Bwana Cecil ameiambia BBC, kuwa kesi hiyo ilifutiliwa mbali kutokana na kile alichokitaja kama ukosefu wa ushahidi wa kutosha dhidi yake.
Mshukiwa huyo alikamatwa mwezi Septemba, kwa kukiuka sheria za hiyo kwa kuonyesha mchezo huo bila kibali wenye maudhui ''The River and the Mountain''
Mapenzi ya jinsia moja imeharamishwa nchini Uganda.
Bunge la nchi hiyo linajadili uwezekano kwa kuimarisha adhabu ya wale watakaopatikana wakijihusisha na mapenzi ya jinsia moja.
Rais wa Uganda akikagua gwaride la kijeshi
No comments:
Post a Comment