Kijana atuhumiwa kunajisi kitoweo
WAKAZI wa Kata ya Bashnet, Wilaya ya Babati,
mkoani Manyara wamelaani kitendo cha mkazi mmoja wa kata hiyo
kuwaingilia mbuzi, na wameitaka Serikali kumchukulia hatua kali za
kisheria.
Baadhi ya wakazi wa eneo hilo wakiwamo wafugaji wamesikitishwa na kitendo hicho cha kijana huyo kuwaingilia mbuzi wao.
Mmoja kati ya wakazi hao, Abraham Mlundi alisema
juzi ni mara ya tano kwa kijana huyo kumuingilia mbuzi wa mkazi mmoja wa
eneo hilo, kitendo ambacho ni kinyume na mila na desturi.
Mlundi alisema imekuwa ni tabia ya muda mrefu kwa
kijana huyo kuwaingilia mbuzi hasa nyakati za jioni na kwamba,
akishafanya kitendo hicho anahama eneo hilo kwenda kujificha vijiji vya
mbali.
“Hadi hivi sasa hatujatambua lengo lake
anapowaingilia mbuzi hao, ingawa wengine wanadai ni vitendo vya
ushirikina na wengine wanahisi anafanya hivyo kutokana na kukosa mke
hajaoa,” alisema Mlundi.
Alisema hii ni mara ya tano kwa kijana huo
kuwaingilia mbuzi na kwamba, wamekuwa wakifanya jitihada kuhakikisha
anakamatwa ili afikishwe kwenye vyombo vya sheria.
“Siku ya mwisho kufanya tukio hilo, kijana huyo
alitaka kuuawa ila alikimbia kwani alikutwa amembana mbuzi kwenye zizi,”
alisema Mlundi.
Hata hivyo, Mtendaji wa Kijiji cha Bashnet, Omary
Mwanditi alithibitisha tukio hilo na kwamba, kijana huyo amekuwa na
tabia ya kuwaingilia mbuzi.
“Tunaendelea kumtafuta kijana huyo kwani vitendo
anavyovifanya siyo vya kiungwana, pia ni kinyume cha ustaarabu kwenye
mila na desturi kwa Watanzania,” alisema.
No comments:
Post a Comment