Polisi wa Nigeria wakishika doria baada ya shambulio
Watu wanne wameuawa nchini
Nigeria, wakati kituo cha polisi na ofisi ya serikali ya mtaa
ilipovamiwa na watu wenye bunduki Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo.
Kwa mujibu wa polisi nchini humo mashambulizi
hayo yamefanywa katika mji wa Song, uliopo karibu na mpaka wa nchi hiyo
na Cameroon.
Msemaji wa polisi wa jimbo la Adamawa, amesema polisi mmoja, mwanajeshi na raia mmoja na mjukuu wake ndio waliofariki.
Ingawa msemaji huyo wa polisi hakulilaumu kundi
lolote kwa mashambulizi hayo, katika siku za hivi karibuni wapiganaji wa
kundi la Boko Haram wamekuwa wakifanya mashambulizi ya mara kwa mara
Kaskazini mwa Nigeria.
Wakazi wa eneo hilo wanasema baadhi ya waliokufa miili yao ilikuwa imeteketezwa kwa moto.
Msemaji wa polisi Mohammed Ibrahim, ameiambia
idhaa ya BBC ya lughya ya Hausa kwamba vikosi vya usalama tayari
vimepelekwa katika eneo hilo.
Ameendelea kusema kwamba mpaka sasa hakuna mshukiwa yeyote aliyetiwa mbaroni.
Wiki iliyopita, kumekuwa na tukio kama hilo katika eneo la Maiha lililopo katika jimbo hilo hilo la Adamawa.
Mashambulizi yanayohusishwa na kundi la Boko
Haram, ambalo linataka sheria za Kiislamu maarufu kama Sharia kuanza
kutumika nchini humo, yashasababisha vifo vya zaidi watu elfu tatu
katika miaka ya hivi karibuni.
No comments:
Post a Comment