Rais wa Ghana akiapishwa
Chama kikuu cha upinzani nchini Ghana, kimesusia sherehe za kuapishwa kwa rais John Mahama kufuatia uchaguzi wa mwezi uliopita uliokumba na utata.
Chama cha New Patriotic Party (NPP) kimedai Bwana Mahama alishinda uchaguzi huo kwa njia ya udanganyifu.
Matokeo rasmi yalimpa Bwana mahama ushindi wa asilimia 50.7, ya kura zaote zilizopigwa, kiwango ambacho kinamfanya kueouka duru ya pili ya uchaguzi dhidi ya mgombea wa chama cha NPP Nana Akufo-Addo, ambaye alipata 47.7%.
Kabla ya kuapishwa kwake rais Mahama alitoa wito kwa rais wa nchi hiyo kuwa watulivu na kuwa na umoja, ili kudumisha demokrasia yao ambayo kwa sasa inakisiwa ndiyo thabiti zaidi barani Afrika.
Bwana Mahama alikuwa makamu wa rais hadi kifo cha ghafla cha rais John Atta Mills mwezi Julai mwaka uliopita.
Kiongozi wa chama cha NPP
No comments:
Post a Comment