Waziri ashangaa ndege kuuzwa Sh500,000
Ndege ndogo
WAZIRI wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mhandisi
Christopher Chiza jana alishikwa na butwaa, pale alipopewa taarifa ya
kuuzwa ndege tatu za Serikali, ambazo zilikuwa katika Kituo cha Kilimo
Anga kwa kiasi cha Sh500,000 kwa kila moja.
Ndege hizo, tatu zilikuwa zikitumika katika udhibiti wa wadudu waharibifu wa mazao .
Akisoma taarifa ya kituo hicho mbele ya Waziri
Chiza, Mhandisi Mkuu wa Ndege wa kituo hicho,Gideon Mugusi,alizitaja
ndege hizo kuwa ni 5H-MRN, Cessna 185 nyingine ni 5H-MRF, Cessna 185 na
nyingine aina ya 5H-MRP piper Super Cub ambazo zilianguka katika
vipindi tofauti.
“Ndege zote tatu ziliharibika lakini Shirika la
Bima la Taifa(NIC), walilipa Serikali kupitia katibu mkuu wa Wizara ya
Kilimo, kulingana na viwango vya bima vilivyokuwa vikilipwa na
wizara”alisema Mugusi.
Hata hivyo alisema tangu kuanguka na kuuzwa kwa
ndege hizo,shughuli za kituo hicho, Kimekuwa zikidorora kwani marobani
karibu wote wameondoka na kituo kimebaki na ndege moja tu ambayo pia ni
mbovu na kibali cha kuruka angani kimekwisha.
Alisema kwa sasa
kutokana na kukosekana kwa ndege, gharama za uendeshaji wa shughuli za
kituo zimekuwa ni kubwa mno kwani wanalazimika kukodisha helikopta na
gharama zake zimekuwa zikipanda mwaka hadi mwaka.
Waziri aja juu:
Kutokana na maelezo hayo, waziri Chiza alikuja juu na kuhoji iweje ndege hizo, ziuzwe kwa Sh 500,000 kila moja.
zinaendelea kufanyakazi na zinamilikiwa na nani,”alisema Chiza.
Waziri
huyo, pia alihoji iwapo ndege hizo, zilifutwa kwenye orodha ya
kumbukumbu za Serikali kama hazifai kwa matumizi pia kama ufutwaji wake
ulifuata sheria na kanuni za Serikali.
“Leo sikuja kukamata mchawi, ila mimi binafsi
nitafuatilia ili kuona kama sheria zilifuatwa au kama ndege zimeuzwa
bila kufuata sheria” alisema Chiza.
Awali alisema Serikali ina mpango wa kufufua kitengo hicho na kwa kuanzia tayari imetoa fedha za kununua ndege moja.
“Naagiza mfanye mchakato haraka wa kununua ndege
hii, hatutaki tena ukiritimba kwani nia ya Serikali ni kufufua kituo
hiki,”alisema Chiza.
Alisema ,kituo hicho ndiyo pekee katika nchi za
Afrika ya Mashariki chenye uwezo wa kutoa huduma hiyo ya kilimo anga na
kama ndege zikianza kufanya kazi, basi zitaweza kukodiwa na nchi
jirani.
Kituo cha Kilimo Anga kilianzishwa na wizara ya
kilimo ,ikishirikiana na Umoja wa Mataifa kupitia Shirika la UNDP na FAO
mnamo mwaka 1979 na lengo kubwa lilikuwa ni kuimarisha utoaji huduma
katika sekta ya kilimo katika kupambana na visumbufu vya mimea
wahamao(migratory pest control).
No comments:
Post a Comment