Na John Banda, Dodoma
BANK ya NMB Kanda ya kati Dodoma imetoa msaada wa madawati 50 wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 5 kwa ajili ya shule ya msingi ya Nkuhungu iliyopo katika Manispaa ya Dodoma.
Akikabidhi msaada huo Meneja wa bank
ya NMB kanda ya kati Gabriel Ole Loibanguti alisema msaada huyo ni moja
ya shughuli zinazofanywa na taasisi hiyo ya kifedha
ambayo imekuwa ikisaidia mambo mbalimbali kwenye jamii kama vile
elimu,afya na michezo.
Loibanguti alisema Bank ya NMB inatambua changamoto kubwa iliyopo katika shule hiyo hasa ya kukosa madawati kwa kipindi
kirefu hali ambayo imewasababishia hata na wanafunzi kuathirika kiakili zaidi.
Meneja
huyo akizungumza katika hafla hiyo alisema kuwa pamoja na upungufu
mkubwa uliopo wa madawati shuleni hapo,ni wakati sasa
taasisi,mashirika,watu binafsi na serikali ikaelekeza misaada yao
kwenye shule ili kupunguza kero zinazowakumba wanafunzi na walimu wao.
Naye Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Godwin Masaki akipokea msaada huo alisema kuwa NMB imepunguza kwa kiasi kero ya wanafunzi karibu wote ya kukaa chini.
Masaki alisema zaidi ya nusu ya Wanafunzi 3012 wa shule ya msingi Nkuhungu katika Manispaa ya Dodoma wanakalia mifuko ya plastiki (maarufu Salufeti) wanapokuwa madarasani kwa sababu za kukosa madawati.kwa kipindi cha miaka kumi na mbili.
Mkuu huyo wa shule alisema kuwa kwa miaka kumi na mbili nusu ya wanafunzi wawanakaa chini ya mifuko ya plastiki kutokana na uhaba mkubwa wa kukosa madawati katika shule hiyo.
"Idadi ndogo ya wanafunzi ndiyo inayokaa kwenye madawati machache yaliyapo,lakini walio wengi wanatandika mifuko yao chini,hali hii inawafanya wanafunzi hao kudumaa kwa akili zao"alisema Masaki.
Aidha alisema uhaba wa madawati hayo unatokana na wanafunzi walio wengi wanatoka katika familia zisizo na uwezo wa kuchangia na wachache waliopo wanatoka kwenye familia ambazo vipato vyao vinaridhisha.
Kwa upande wao wanafunzi wa shule hiyo wakizungumzia tatizo hilo lililopo shuleni hapo walisema kuwa tatizo la upungufu wa madawati linatokana na wingi wa wanafunzi waliopo.
Neema Kasimu (16) ambaye ni mwanafunzi wa darasa la saba,alisema kuwa wingi huo unasababisha pia kukosekana kwa shule nyingine katika eneo hilo la Nkuhungu hivyo kuwafanya wakazi wote kutegemea hapo.
"Hali hii ndiyo maana kwa kipindi karibu miaka kumi na mbili watoto wote tunakaa chini kuanzia darasa la tatu hadi la saba wanafunzi wote tunakaa chini huku tumetandika mifuko ya plastiki"alisema mwanafunzi huyo kwa machungu.
Neema alisema kuwa tunapoondoka nyumbani tunabeba mifuko hii unayoiona kwa ajili ya kukalia chini ili tusichafue nguo zetu,hii inatusikitisha na hata hivyo tunaishukuru bank hii ya nmb kwa kutupunguzia kero ya kukaa chini.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment