Viongozi wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Sheikh Ponda Issa
Ponda (Kushoto) na Katibu wake,Sheikh Mukadam Swalehe wakiwa katikati ya
askari magereza kwenye majengo ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,
jijini Dar es Salaam
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es
Salaam, imetathmini ushahidi wa upande wa mashtaka yanayowakabili watu
54, wanaodaiwa kuwa wafuasi wa Kiongozi wa Jumuiya na Taasisi za
Kiislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda na kubaini kuwa wana kesi ya kujibu.
Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka ya
kula njama, kufanya maandamano yaliyozuiliwa na polisi, kukusanyika
isivyo halali , uchochezi na kusababisha uvunjifu wa amani.
Hayo yalisemwa jana na Hakimu Mkazi, Sundi
Fimbo ambaye alisema baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na mashahidi
10 wa upande wa mashtaka na vielelezo , mahakama imeona kuwa washtakiwa
wote wana kesi ya kujibu na kwamba wanapaswa kutoa utetezi wao.
Mapema wakili wa washtakiwa hao, Mohammed
Tibanyendera aliiomba mahakama iwaachie huru washtakiwa kwa madai kuwa
ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka, umeshindwa kuthibitisha
makosa dhidi ya washtakiwa.
Wakili Tibanyendera alidai kuwa, mashahidi wa
upande wa mashtaka wote walikiri kuwa hakuna hata mmoja aliyewahi kuona
tangazo la kuzuia maandamano.
Pia alidai kuwa hakuna ushahidi
uliowasilishwa na upande wa mashtaka ukionyesha kuwa kulikuwa na
maandamano na kwamba mashahidi wote waliithibitishia mahakama kuwa
walishiriki katika kukamata washtakiwa kwa njia ya simu ya upepo ya
polisi.
Wakili huyo pia alidai kuwa mikusanyiko
haikuwa ya kuvunja amani na kwamba wala hakuna shahidi hata mmoja
aliyeieleza mahakama kuwa alishuhudia uvunjifu wa amani ama malalamiko
kutoka kwa majirani kuhusu hofu.
“Hii inadhihirisha kuwa mkusanyiko waliokuwa
nao washtakiwa ulikuwa halali na hakukuwa na amri yoyote ile ya kuzuia
watu kukusanyika katika Jamhuri ya Tanzania hapo Februari 15, mwaka
huu,” alidai wakili huyo.
Pia wakili huyo wa kujitegemea alidai kuwa
hakukuwahi kutolewa wakati wowote ule, amri ya kuzuia mkusanyiko na
kwamba walizuia maandamano.
Wakili Tibanyendera alidai kuwa ukamataji
wa wateja wake, ulifanyika baada ya Swala ya Ijumaa, na kwamba watu
walikamatwa katika maeneo mbalimbali yakiwemo ya Mkunguni na Makunganya.
Alifafanua
kuwa waliokamatwa katika maeneo ya Mkunganya walikamatwa umbali wa mita
100 kutoka msikitini, DIT walikuwa karibu na kituo cha daladala na
waliokamatwa katika eneo la Mkunguni walikuwa karibu na misikiti
takriban mita tatu.
“ Huu ni uwiano mkubwa wa kimazingira,
tulitarajia tutapata ushahidi tofauti baina ya watu waliotenda kosa na
waliokusanyika katika nyumba za ibada,” alidai wakili huyo wa utetezi.
Baada
ya kumaliza kutoa hoja hizo, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Benard
Kongola aliiomba mahakama iwaone washtakiwa kuwa wana kesi ya kujibu.
Hakimu Fimbo aliiahirisha kesi hiyo hadi leo washtakiwa watakapoanza kujitetea.
Hatua
hiyo ilifikiwa baada ya upande wa mashtaka kupitia mawakili wa Serikali
waandamizi, Benard Kongola, Nassor Katuga na Joseph Mahugo kufunga
ushahidi wao.
Upande wa mashtaka ulifunga ushahidi wake baada ya
kupeleka mashahidi 10 mahakamani kutoa ushahidi dhidi ya washtaka
wakiambatanisha pia vielelezo 12.
Alidai kuwa Februari 11, mwaka huu alipokea
barua kutoka katika Shura ya Maimamu, ikimwomba kibali cha kufanya
maandamano ya kwenda ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).
Alidai kuwa barua hiyo ilisainiwa na Sheikh
Juma Idd na kwamba ndani yake pia ilikuwa inahoji sababu za kutokumpatia
dhamana Sheikh Ponda .
Pia walikuwa wakitaka maandamano hayo, yafanyike Februari 15,
mwaka huu baada ya Swala ya Ijumaa na waandamanaji watakuwa wakitokea
katika misikiti mbalimbali.
ACP Msangi alidai kuwa yeye na maofisa wenzake, walitafakari barua hiyo ili kujua uzito wa maandamano hayo.
Alidai kuwa Jeshi la Polisi lilibaini kuwa
halikuwa na askari wa kutosha kuwapeleka katika kila msikiti kwa ajili
ya kuwalinda waandamanaji.
No comments:
Post a Comment