Hugo Chaves
Venezuela. Serikali ya Venezuela imesema kuwa
ipo mbioni kuanza uchunguzi rasmi ili kuchunguza kwa kina kama ugonjwa
wa saratani aliokuwa nao Rais Hugo Chavez umesababishwa na maadui wa
kigeni.
Kauli hiyo ilitolewa na aliyekuwa Makamu wa
Chavez ambaye kwa sasa aliteuliwa kuwa rais wa muda Nicolas Maduro
aliahidi kuanzisha uchunguzi ili kuchunguza madai yaliyotolewa na watu
wengi akiwemo Chavez mwenyewe kwamba maradhi yaliyokuwa yakimsumbua hadi
kusabisha kifo chake yalitokana na sumu aliyopewa.
Maduro alisema Serikali ya Caracas itawaalika
wanasayansi wa nchi za nje kushirikiana na kamati ya nchi hiyo ili
kuchunguza tuhuma hizo.
Rais Hugo Chavez wa Venezuela alifariki dunia tarehe 5 mwezi huu baada ya kuuugua saratani kwa muda wa miaka miwili.
Kwa sasa serikali ya nchi hiyo ipo chini ya
Nicolas Maduro aliyekuwa makamu wa rais chini ya Rais hugo Chaves licha
ya kuwa serikali ilimkabidhi madaraka vyama vya upinzani vilipinga suala
hilo kwa madai kuwa lipo kinyume na sheria ya nchi hiyo.
Hugo Rafael Chavez Frias alizaliwa Julai 28,
1954. Alishika madaraka ya kuiongoza Venezuela mwaka 1999. Kufuatia
itikadi yake ya kisiasa ya Kibolivarian na “Usoshalisti wa karne ya 21”,
amelenga katika kutekeleza mageuzi ya usoshalisti katika nchi kama
sehemu ya mradi wa kijamii inayojulikana kama Mapinduzi ya Wabolivia,
ambayo yameshuhudia utekelezaji mpya wa katiba, demokrasia shirikishi na
kutaifisha viwanda kadhaa muhimu.
No comments:
Post a Comment