Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Uratibu na Bunge), William
Lukuvi (kulia) akizungumza na wabunge wa Chadema baada ya kikao cha
kunge kualishwa jana mchana.
Dodoma.Wabunge watano wa Chadema jana
walitimuliwa bungeni na kuamriwa kukaa nje ya Bunge kwa siku tano
kutokana na vurugu zilizotokea jana usiku.
Wabunge hao ni Lissu, Hezekiah Wenje (Nyamagana),
Highness Kiwia (Ilemela), Joseph Mbilinyi (Mbeya Mjini) Godbless Lema
(Arusha Mjini) na Mchungaji Peter Msigwa (Iringa Mjini).
Chanzo za kufukuzwa kwao ni kuwazuia askari wa
Bunge kumtoa nje Lissu ambaye alikuwa ameamriwa kutoka nje na Naibu
Spika, Job Ndugai baada ya kuingilia hotuba ya Mbunge wa Iramba
Mashariki, Mwigulu Nchemba.
Kutokana na tafrani hiyo, Nchemba hakuweza
kuhitimisha hotuba yake hivyo Ndugai alilazimika kukatisha mkutano wa
Bunge.Hata hivyo wakati akiahirisha mkutano huo, tayari wabunge hao
walikuwa wameshatolewa nje baada ya askari kuongezwa.
Mapema Mbunge wa Kigoma Mjini (CCM), Peter
Serukamba alitoa tusi zito la nguoni wakati wa hotuba ya Msemaji Mkuu wa
Kambi ya Upinzani kwa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma,
licha ya Spika wa Bunge, Anne Makinda kupiga mkwara wa kuwashughulikia
wabunge watakaorusha matusi.
Mbali na tukio hilo Lema naye alichafua hali ya
hewa baada ya kuwatuhumu viongozi wa CCM akiwamo Rais Jakaya Kikwete kwa
udini, madai ambayo Bunge limempa siku saba kuyathibitisha.
Lema aliituhumu CCM na Serikali yake chini ya Rais
Kikwete kwa kushindwa kutatua mgogoro wa kidini na badala yake kuwa
kama analikwepa tatizo. Alionya kuwa Taifa linapasuka kwa migogoro
kutokana na viongozi wa Serikali kushindwa kulishughulikia.
Kauli iliwanyanyua vitini Waziri wa Nchi katika
Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Uratibu na Sera), William Lukuvi na
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema.
Lukuvi na Jaji
Werema walisimama wakidai kuwa Lema alikuwa amemdhihaki Rais Kikwete kwa
kauli zake za kumhusisha na masuala ya udini.
Hata hivyo, Mnadhimu Mkuu wa Upinzani, Lissu
alisimama kumtetea Lema akidai hakuwa amemdhihaki Rais bali alikuwa
amemkosoa kitu ambacho kanuni za Bunge zinaruhusu.
Lema aliruhusiwa kuendelea na hoja yake na ndipo
akamtolea mfano Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu),
Steven Wassira wakati alipokwenda Mwanza kutatua mgogoro baina ya
Wakristo na Waislamu kuhusu suala la kuchinja.
“Wassira akifahamu yeye ndiye, Waziri alikwenda
Mwanza na kuwaacha viongozi wa dini za Kikristo na Kiislamu watatue
wenyewe suala la kuchinja. Sasa alitaka diwani atatue mgogoro ule?”
Baada ya kumaliza kuchangia, Naibu Spika
alitangaza kuwa Lema anatakiwa kuwasilisha katika muda wa siku saba
uthibitisho kuwa Rais anahusika na tati
Serukamba
Serukamba alipewa nafasi ya kutoa
taarifa wakati wabunge walipokuwa wakilumbana juu ya uhalali wa Msemaji
wa Upinzani, Profesa Kulikoyela Kahigi kuzungumzia bungeni masuala
yaliyoko mahakamani na shughuli za Idara ya Usalama wa Taifa.
Wakati akijiandaa kusoma vifungu vya kukatiza
hotuba ya Profesa Kahigi, alitukana tusi zito la nguoni kwa lugha ya
kimombo ambalo kwa sababu za kimaadili hatukuweza kuliandika, kisha
akaendelea kuzungumza huku baadhi ya wabunge wakipigwa butwaa.
Hata hivyo, Naibu Spika, Job Ndugai aliyekuwa
akiongoza shughuli za Bunge wakati huo, hakutoa karipio lolote huku
akimruhusu Serukamba kuendelea kwa muda kabla ya kumkatiza na kumruhusu
Mbunge wa Simanjiaro (CCM), Christopher Ole Sendeka kuzungumza.
Ubishi ulivyoanza
Muda mfupi
kabla ya Profesa Kahigi kuanza kusoma hotuba yake, Serukamba alisimama
na kuomba mwongozo wa Spika kupitia Kanuni ya 68(1) akitaka isisomwe
kuanzia ukurasa wa kwanza hadi wa nne kwa kuwa unaingilia uhuru wa
Mahakama... “Ni juzi tu Akoonay (Mustapha, Mbunge wa Mbulu - Chadema),
alitukumbusha kwamba mambo hayo ni ‘prejudice’ kwa Mahakama kwa hiyo
ukiruhusu hilo Naibu Spika itakuwa ni ajabu.”
Kabla Naibu Spika hajatoa mwongozo wake, alimtaka
Profesa Kahigi kuzungumza kama anakubaliana na Serukamba, lakini Profesa
Kahigi alisema anaomba kuendelea kusoma hotuba yake kama ilivyo.
Baadaye Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika
aliomba kumpa taarifa Serukamba kwamba katika kurasa alizozitaja hakuna
jambo lolote lililopo mahakamani hivyo aangalie vizuri.
“Mheshimiwa Naibu Spika napenda kumpa taarifa mtoa
taarifa kwamba hakuna lolote lililopo mahakamani, ukurasa wa kwanza
unazungumzia Idara ya Usalama wa Taifa, haipo mahakamani, ukurasa wa
pili umemtaja Dk Stephen Ulimboka, halipo mahakamani hivyo hakuna lolote
lililopo mahakamani,” alisema.
Baada ya hapo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu
(Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi alisimama na kueleza kuwa
aliyoyasema Serukamba ni kwamba hotuba hiyo inafanya kesi iliyopo
mahakamani kuwa ya kisiasa akisema... “Kifungu cha 16 cha Sheria ya
Usalama wa Taifa hakiruhusu watumishi wa Usalama wa Taifa kutajwa humu
ndani wala kuchapishwa popote.”
Naibu Spika alisimama na kusema jambo hilo
limeshajitokeza ndani ya Bunge na Akoonay alishawakumbusha kuwa ni
kuingilia Mahakama.
“Jambo hili lilishaleta kasheshe humu ndani
na ruling (uamuzi) ya hili ilishatolewa na Spika, ‘ruling’ yangu ni
kwamba kuanzia ukurasa wa kwanza mpaka wa nne, mambo ya Dk Ulimboka,
Usalama wa Taifa na Lwakatare.........,” aliishia hapo Ndugai na
kuwaruhusu Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, Mbunge wa Singida Mashariki,
Tundu Lissu, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Angela Kairuki na Ole
Sendeka kuzungumza.
Mdee alisema ukurasa wa kwanza mpaka wa tatu wa
hotuba hiyo hakuna sehemu jina la Lwakatare lilipotajwa na kwamba
ukurasa wa nne uliotaja jina la Lwakatare hauzungumzii mwenendo wa
kesi... “Hoja anazoleta Lukuvi atusomee hiyo Sheria ya Usalama na
atuelezee na alinganishe na kilichopo hapa.”
Mdee aliungwa mkono na Lissu aliyesema kuwa sheria
anayozungumzia Lukuvi ipo lakini haikatazi kutajwa majina ya
wanausalama ndani ya Bunge... “Ninayo hiyo sheria hapa ya mwaka 1996,
haya maneno kwamba Sheria ya Usalama inakataza masuala ya Usalama wa
Taifa kutajwa ni uchochezi. Hicho kinachoelezwa kukataza ‘disclosure’
(kuwataja) ni huko nje na si humu ndani.”
Lissu alisema sheria hiyo inakataza kuchapishwa majina hayo nje ya Bunge na si vinginevyo.
Kairuki alipingana na Lissu akieleza kuwa
amepotosha kwa kuwa sheria hiyo ya Usalama wa Taifa hairuhusu kuwataja
watumishi wake bila kuomba ruhusa kwa waziri.
“Lissu anapotosha kwa kuwa hairuhusiwi mtu yeyote
kuchapisha jina la mtumishi wa Usalama wa Taifa bila kuomba ruhusa kwa
waziri,” alisema Kairuki.Ndipo Naibu Spika alipompa tena nafasi
Serukamba na alipoanza tu kuchangia kuliibuka maneno ya chinichini
ambayo yalionekana kumkera ndipo alipotoa neno hilo zito.
Baadaye Ndugai alisema kwa kuwa hilo suala ni la kikanuni, anaiagiza Kamati ya Kanuni ikutane ili tujadili suala hilo.
Katika hotuba hiyo ambayo awali, waandishi
walipata nakala yake, Profesa Kahigi alikuwa ameandika mambo mbalimbali
yanayohusu kutekwa na kuteswa kwa Kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari
Tanzania, Dk Steven Ulimboka na masuala mengine yanayohusiana na kesi ya
ugaidi inayomkabili Mkurugenzi wa Usalama wa Chadema, Wilfred
Lwakatare.
zo la udini.
No comments:
Post a Comment