Tabora. Mwenyekiti wa Chadema,
Freeman Mbowe amemwagiza Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe kuhakikisha
chama kinapata ushindi katika majimbo mengi kwenye uchaguzi mkuu ujao.
Mbowe alisema chama chake kitahakikisha kinachukua
majimbo ya Samwel Sitta, (Urambo Mashariki), Ismail Aden Rage (Tabora
mjini) na Jimbo la Kaliua la Profesa Juma Kapuya, katika uchaguzi mkuu
ujao mwaka 2015.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara, Mbowe
alimwagiza mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini kuhakikisha kwamba majimbo
hayo yanachukuliwa na Chadema katika uchaguzi mkuu ujao.
Alimtaka kufanya kampeni za mtaa kwa mtaa, nyumba kwa
hadi
nyumba na mtu kwa mtu ili kuhakikisha kwamba wabunge hao wa sasa katika
majimbo hayo hawachaguliwi tena na wananchi katika uchaguzi huo.
Katika mkutano huo uliofanyika kwenye Uwanja wa
Shule ya Msingi Town School mjini Tabora, pamoja na mambo mengine
alisema anazindua kampeni hiyo kwa ajili ya mikoa ya Tabora, Kigoma na
Katavi ambapo Zito Kbwe alikabidhiwa jukumu la kuisimamia kanda hiyo.
Aliwageukia polisi na kuwataka kukiunga mkono
chama hicho ili kikifanikiwa kuingia madarakani kiweze kuwaboreshea
mishahara yao kuliko ilivyo sasa akidai wanalipwa mishahara kiduchu
ikilinganishwa na ugumu wa kazi yao.
“Nyie makamanda nanyi mmepigika kama sisi, sasa
ninachowaomba tuungeni mkono kupambana na hawa CCM ili tuwakomboe
wanyonge,” alisema Mbowe.
Awali Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Zitto Kabwe
alisema Kanda ya Magharibi ina historia katika nchi kwa Mkoa wa Tabora
kuwa kitovu cha mapambano ya uhuru wa nchi na Kigoma kuwa kitovu cha
mapambano ya mageuzi.
No comments:
Post a Comment