Mahakama nchini Afrika
Kusini imemhukumu kifungo cha miaka arobaini raia mmoja wa Thailand
aliyepatikana na hatia ya kuuza pembe za vifaru na kuandaa maonyesho ya
uwindaji yasiyokubalika
Chumlong Lemtongthai alikiri kosa la kuwalipa makahaba kuweza kufanya maonyesho ya uwindaji wa vifaru.
Pembe hizo ziliuzwa barani Asia ambako soko la pembe hizi ni kubwa sana kwani hutumiwa kama dawa.
Zaidi ya vifaru miatano wameuawa nchini humo na wawindaji haramu mwaka huu pekee.
Akitoa hukumu hiyo jaji alisema kuwa hataki wajukuu wake wakuwe bila kujionea vifaru nchii humo.
No comments:
Post a Comment