Watu
watano wanaosadikiwa kuwa majambazi wakiwa na bunduki na mabomu ya
kienyeji wamevamia Ofisi za Taasisi ya kutoa huduma za mikopo ya
Financial International Asisstance (FINCA) mjini Geita na kuambulia
kupora kompyuta mpakato mbili na kuzikosa Sh milioni 19 zilizokuwa
zimehifadhiwa kwenye ofisi hiyo.
Katika tukio hilo lililotokea usiku wa
kuamkia jana majambazi hayo pia yamemjeruhi kwa risasi mlinzi wa kampuni
ya Security Group ambaye amelazwa katika hospitali ya wilaya ya Geita.
Akithibitisha kuwepo kwa tukio hilo,
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Leonard Paulo, alimtaja mlinzi
aliyejeruhiwa kuwa ni Rajabu Muhoja (28).
Akifafanua alisema kuwa Askari polisi
waliokuwepo doria walikwenda eneo la tukio baada ya kusikia kelele za
mlinzi aliyekuwa akikabiliana na majambazi hayo, ambayo baadaye
yalifanikiwa kukimbia.
Alisema jeshi a polisi linaedelea na
upelelezi na baadhi ya vilelezo yakiwemo mabaki ya risasi pamoja na
viroba viwili vya mchanga wa kutengezea milipuko vimehifadhiwa kwa
uchunguzi.
Wakizungumzia tukio hilo, baadhi ya
wananchi wamedai kuwa kabla ya kuanza kusikia milio ya risasi na
milipuko ya baruti kulitanguliwa na milio ya tahadhari.
Hata hivyo, walisema hawakutambua ilikuwa
inaashiria nini hadi milio ya risasi ilipoanza kusikika na ikidaiwa
kudumu kwa zaidi ya nusu saa ambapo mabaki tisa ya maganda ya risasi
yamepatikana eneo la tukio na risasi mbili ambazo hazijatumika.
Esther John mmoja kati ya maafisa mikopo wa Taasisi hiyo alisema kuwa kompyuta zilizoibwa zilikUwa na kumbukumbu ya mikopo.
No comments:
Post a Comment