Serekali yawataka waisramu kuacha ushabiki

Na John Banda, Dodoma

WAAUMINI wa dini ya kiislamu nchini wametakiwa kuacha kushabikia mvurugano wa kidini ulipo hivi sasa bali wawe mstari wa mbele katika kuhamasisha amani na utulivu kwa Watanzania.

 

Rai hiyo ilitolewa jana na Naibu Waziri wa Tawala za mikoa na Serikali za mitaa (Tamisemi) Kassim Majariwa wakati alipokuwa akihutubia waumini wa dini hiyo wakati wa mahafali ya wahitimu wa masomo ya kiarabu, kopyuta na cherehani yanayotolewa na kituo cha Gadaffi mjini hapa.

 

Majaliwa alisema kuwa waislamu hawana budi kuwa mastari wa mbele kuondoa tofauti zilizopo hivi sasa ili kuweza kuleta mshikamano na umoja ambao umekuwepo kwa mda mrefu nchini.

 

Alisema kuwa hakuna haja ya watanzania kuwa na mifarakano isiyo kuwa natija katika masuala ya kidini, kiitikadi wala kikabila kama ambavyo hivi sasa imekuwa ikijitokeza katika maeneo mbalimbali.

 

“Hatuna budi kuacha mvulugano wa kidini ulipo hivi sasa na kuwa mabalozo wema katika kuhamasisha amani umoja na mashikamano… kwani mvurugano uliopo kwa sasa hauna tija” alisema Majaliwa.

 

Aidha alitoa wito kwa wahitimu hao kujiunga katika vikundi vya uzalishaji mali ili waweze kupata mikopo watakayo itumia katika kuanzisha miradi mbalimbali inayo weza kuwainua kiuchumi.

 

“ Mkiwa katika vikundi mnaweza kuwa na uwezo kukopa pesa kwajili ya kuanzisha miradi yenu mbalimbali kupitia mafunzo mliyapata hapa”alisema.

 

Aliushari uongozi wa kituo hicho kuongeza kozi ya ujasiriamali ambayo itaweza kuwasaidia vijana wanaohitimu katika kozi mbalimbali kituoni hapo kuweza kuwa na uwezo wa kubuni miradi yenye tija.

 

“Elimu ya ujasilimali ndio msingi wa mambo yote kama kijana atakuwa nayo naweza kuanzisha mradi ambao ataweza kuusimamia na kufanikiwa” alisema

 

Hata hivyo aliowataka wazazi kuwasisitiza watoto wao kujitokeza kwa wingi katika kuitumia fursa hiyo ya kupata mafunzo katika fani mbalimbali.

 

“Hapa wanatoa bure mafunzo yao wakati katika maeneo mengine ni lazima ulipe hivyo basi wahamasisheni watoto waje kwa wingi ili waweze kujifunza”.

 

Jumla ya wanafunzi 217 waliohitimu mafunzo ya  Lugha kiarabu, , kopyuta na cherehani.


Mwisho.

No comments:

Post a Comment